ZITTO AUNGURUMA JIJINI MBEYA

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe akiwatubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo  jijini Mbeya.

Na Mwandishi wetu-Mbeya

ACT Wazalendo inaendele na ratiba yake ya kufanya mikutano katika mikoa mbali mbali kama walivyotoa ratiba yao wiki iliyopita, leo tarehe 21.06.2015 wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara jijini Mbeya katika uwanja wa Rwandanzovye.

"Azimio la Tabora ni mpango mkakati wa kisiasa wa kurejesha miiko ya uongozi ambayo imepuuzwa na kutupiliwa mbali na wanasiasa na viongozi wa leo kiasi ambacho wizi na ufisadi wa mali ya umma imekuwa ni mambo ya kawaida. Hii haikubaliki". Alisema Zitto Kabwe.

Lengo kuu la mikutano ya ACT-Wazalendo ni kuzindua Azimio la Tabora lililohuisha msingi ya Azimio la Arusha na sera iliyoboreshwa ya Ujamaa wa Kidemokrasia. Pamoja na kuitangaza sera ya chama chao ambayo ni, misingi ya Uzalendo, Uwazi, Uwajibikaji, Uadilifu, Usawa, Hifadhi ya Jamii, Umoja, Utu, Kujitegemea, Bidii na Weledi katika kazi.

                                                Wananchi wakifuatilia mkutano jijiniMbeya.





About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment