WAFANYAKAZI 21 WA KAMPUNI YA KUCHIMBA DHAHABU YA ACACIA WAPANDA MLIMA KILIMANJARO KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Acacia,wanafamilia pamoja na marafiki wa kampuni hiyo wakishuka kutoka katika gari tayari kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro .
Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya Acacia,Brad Gordon akitelemka kuanza changamoto ya kupanda mlima Kilimanjaro kama njia ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini.
Meneja wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Kampuni ya Acacia,Necta .P.Foya akifunga vizuri mizigo yake kabla ya kuanza safafti ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya kuchimba dhahabu,Brad Gordon akifurahia jambo na mwakilishi wa kampuni ya utalii ya Zara Tour.
Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya Acacia ,Brad Gordon akizungumza na Meneja wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Kampuni ya Acacia,Necta .P.Foya kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro,kulia ni Fredrick Njoka mmoja wa watumishi wa Acacia.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Acacia na familia zao wakitia saini katika makoti kama kumbukumbu ya kundi la kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia elimu nchini kupitia mpango wa CanEducation ulioanzishwa na kampuni ya Acacia.
Afisa mtendaji mkuu wa Acacia,Brad Gordon akitia saini katika makoti hayo.
Meneja wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa kapni ya Acacia,Necta Foya akitia saini katika moja ya makoti hayo.
Kundi la watu 21 kutoka kampuni ya Acacia wakifanya zoezi la uandikishaji kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwalengo la kuchangisha fedha.
Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Acacia,Brad Gordon(katikati) akizungumza kuhusu mpango wa kampuni hiyo kupanda Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya kuhasisha uchangiaji wa elimu nchini kwa lengo la kuchangisha kiasi cha sh za kitanzania Mil 400 ambapo kampuni hiyo katika kila shilingi Moja itakayochangwa itajazia shilingi moja.
Kaimu Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Charles Ngemba akizingumza katika hafla fupi ya kuiaga timu ya watu  21 walioanza safari ya kupandaMlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro,Eva Mallya akisalimia katika hafala hiyo.
Badhi ya wapandaji .
Baadhi ya wapandaji wakiimba kabla ya kuanza zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro.
Neta na Fredy wakipata kikombe cha chai kabla ya kuazna zoezi.
Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya kuchimba dhahabu ya Accacia ,Brad Gordon akiongoza timu ya watu 21 wakiwemo wafanyakazi,marafiki na familia za wafanyakazi wa kampuni hiyo ,kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchangia sekta ya elimu
Safari ya kuelekea kilele cha Uhuru,Mlima Kilimajaro ikianza kushika kasi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment