HATIMAYE 18 WAPITA MCHUJO WA KWANZA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015

Baadhi ya Majaji wakijiandaa kutangaza Rasmi Matokeo ya washiriki 18 walioingia katia Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Kutoka kulia ni Dora Myinga Mkulima na Mjasiliamali, Mwandiwe Makame Mkulima na Mfugaji, Roselyn Kaihula kutoka Ekama Development
 Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam, Eluka Kibona akiwakaribisha majaji kutangaza matokeo ya washindi
 Zephaniah Muggitu a ambaye pia alikuwa ni Jaji  Akieleza kwa ujumla Jinsi mchakato wa kuwapata washindi hao ulivyokuwa
 Bw. Jairos Mahenge ambaye Pia alikuwa ni Mmoja wa Majaji akizungumzia kwa ufupi changamoto walizokutana nazo wakati wa Mchakato mzima wa kuhakiki fomu za kuwapata washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula.
 Ofisa Mahusiano ya Ushawishi  wa Oxfam Tanzania Suhaila Thawer akitoa maelezo mafupi ya Jinsi watakavyo watembelea washindi 18 katika maeneo walipo ili kuona shughuri zao na baadae kuwapata washiriki 15 ambao ndio wataingia katika mshike mshike wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015
Dora Myinga ambaye pia alikuwa ni jaji akiwataja washindi 18 walioingia katika shindano la safari ya kumpata  Mama shujaa wa Chakula
Baadhi ya majaji wakiwa wanaendelea na kazi wakati wa kuwatangaza washindi walioingia kuanza safari ya kumsaka Mama Shujaa wa Chakula 2015
*****
Baada ya zoezi la kupokea na kusahihisha fomu za washiriki wa shindano la mama shujaa wa chakula 2015 kukamilika, takribani washiriki 18 kutoka mikoa tofauti nchini wamefanikiwa kupita katika mchujo wa kwanza kabla ya washiriki watatu kuyaaga mashindano hayo na kubakia 15 ambao ndiyo wataingia kijijini kwa ajili ya kumpata mshindi.

akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa majaji waliohusika katika zoezi la kusahihisha fomu za washiriki, Zephania Mugittu alisema kuwa idadi ya washiriki waliowasilisha fomu zao ni 26,500 ambapo fomu zilizokidhi viwango zikiwa 2,317 tu.

Jaji huyo aliongeza kuwa fomu za washiriki 21 ndiyo zilizovuka alama zaidi ya asilimia hamsini huku vigezo vya umri, shughuli za kilimo cha mazao ya chakula, uvuvi na ufugaji vikiwabakiza washiriki 18 wenye alama za juu kutoka mikoa tofautitofauti.

Naye Ofisa Mahusiano ya Ushawishi  wa Oxfam Tanzania  Suhaila Thawer alimalizia kwa kusema washiriki 18 wote  watatembelewa maeneo waliyopo kuhakikisha kama wanafanya kazi hizo kweli na baadae kuanza rasmi mchakato wa kumpata Mama Shujaa wa Chakula 2015.

Washiriki hao 18 ni Getrude Bundala Deonatus(35) Ukerewe Mwanza, Winnie  L. Mallya (24) Kilimanjaro Moshi, Dina Samwel Sumari (62) Meru Arusha, Tatu Ramadhani Kilua (48) Lushoto Tanga, Edna Gabriel Kiogwe (40) Ilala Dar es salaam, Neema Hilonga (35) Hanang  Manyara,  Pili Kashinje Itamba (30) Kaskazini(U), Eva Mageni Daudi (31) Bagamoyo Pwani, Hawa Athumani  Mkata (56) Masasi Mtwara, Wandutha Daud Kitoelth (48) Mkalama Singida, Shida Daudi Mwedugo (35) Chamwino Dodoma, Hellen Materu (36) Iringa Mjini, Upendo Paulo Mhomisoli (35) Njombe, Savera  Xeveri Mutahyabarwa (65) Bukoba Mjini Kagera, Carolina Humphrey Chelele (48)  Kilombero Morogoro, Stella Fabian  Masulya (42) Ukerewe Mwanza,  Regina Kapili Stephano (19)  Mpanda  Katavi, Rehema Daniel  Lukali (46) Sumbawanga Rukwa.

WEKEZA KWA WAKULIMA WANAWAKE WADOGO WADOGO INALIPA 
 
 

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment