Sheikh Sharifu Msopa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo Hoteli ya Shamoloon iliyopo Sinza kuhusu maombi hayo maalumu.
Sheikh Sharifu Msopa (kulia), akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo Hoteli ya Shamoloon iliyopo Sinza kuhusu maombi hayo maalumu. Kshoto ni Sheikh Maulana Salim.
Sheikh Maulana Salim (kushoto), akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali na bloggers
wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
SHEIKH Sharifu Msopa ametoa ofa kwa viongozi na wananchi nchi nzima ya kuwafanyia maombi pamoja na kuwapaka mafuta maalumu ya uponyaji kutoka Guba ya Uajemi.
Sharifu Msopa ametoa ofa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, ambapo alisema walengwa zaidi ni watu maskini, viongozi mbalimbali wale waliotangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu.
Alisema lengo la maombi hayo ambayo hayachagui dini ni kuwapata viongozi waliochaguliwa na mungu ambao wataliongoza taifa wakiwa na hofu ya mungu.
"Maombi tutakayofanya hayambagui mtu na dini yake kwani tumekuwa tukitoa huduma hii ya maombi bure kwa kushiriana na wenzetu wa kristo na tayari baadhi ya viongozi tumeanza kuwafanyia maombi na yule aliyetayari awasiliane nasi" alisema Sharifu Msopa.
Msopa alisema suala hilo la imani ni muhimu sana hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu na kuwa lengo kubwa ni kuona nchi inapata viongozi waliobora na si bora viongozi kupitia maombi yao.
Alisema baada ya kufanyiwa maombi mtu husika atapakwa mafuta ya ajabu kutoka Guba ya Uajemi ambayo yananguvu ya kuondoa mikosi, uchawi na kumletea bahati muombewaji.
Alisema hivi sasa wapo katika maombi ya mwezi mzima ya kuwaombea, viongozi wa siasa serikali, wafanyabiashara, maskini na makundi mengine ili wapate neema hiyo.
Msopa alisema anaamini kuwa kupitia maombi kiongozi mzuri atapatikana kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na urais na kuwa mara baada ya mtu husika kupakwa mafuta hayo kama atakuwa na uchawi, nuksi na mambo mengine yatamtoka kwa njia ya kuharisha, kutapika na kumfanya awe huru.
Alisema maombi hayo anatarajia kuyafanya nchi nzima kwa kukutana na makundi ya watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi.
Alisema kwamba maombi kama hayo amekuwa akiyafanya katika nchi mbalimbali duniani na yamewasaidia watu wengi kutoka dini zote za kikrito na waislamu na amekuwa akiyafanya bure. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
0 comments :
Post a Comment