LOWASSA AZOA WADHAMINI 3,000 GEITA, CHATO NAKO APATA WA KUTOSHA

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa,(katikati), akipungia mkono maelfu ya wana CCM na wananchi wengine waliofika kwenye ofisi za CCM wilayani Geita Juni 8, 2015, kwa nia ya kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015;
Wakazi wa wilaya ya Geita, wakiwa juu ya nyumba na juu ya mti (picha ya chini), ili kumuona Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa, alipowasili kwenye ofisi za CCM wilayani Geita, Juni 8, 2015 kuomba wana CCM wamdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015
Umati wa wana CCM waliofika kumdhamini Lowassa, na ananchi wengine waliofika walau kumuona wakiwa wamefurika nje baada ya ukumbi wa mikutano ofisi ya CCM wilayani Geita "kutapika" 

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge a Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipokea fomu za udhamini za CCM baada ya ,kujazwa na wananchama wa CCM wilaya ya Geita, kwenye ukumbi wa CCM wilayani humo Juni 8, 2015. Mheshimiwa Lowassa, amedhaminiwa na jumla ya wanachama 3,000 wilayuani hapo
Waziri Mkuu a zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Losassa, akiwaaga wananchi na ana CCM waliofika kumdhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya Chato Juni 8, 2015.
Lowassa akiteremka kutoka ndani ya ndege, kwenye uwan ja mdogo wa mdege a mgodi wa Geita (GGM)
Lowassa, akiwapungia wana ccm waliofika kumdhamini baada ya kukabidhiwa fomu za udhamini zilizojazwa. Jumla ya wana CCM 3,000 walijitokeza kumdhamini
Wana CCM waliofurika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za chama hicho ilayani Geita, wakimshangilia Lowassa
Lowassa, akiondoka huku akiwa amezungukwa na umati wa watu nje ya ofisi za CCM wilayani Geita.
 (Picha zote na K-VIS MEDIA)

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment