Kampuni ya Dodsal Group Dubai
- Tahadhari kwa Wataalam wote
- Tahadhari kwa wafanyakazi wote
- Tahadhari kwa Mr. Rajen Kilachand, Mwenyekiti wa Dodsal Group Dubai
- Tahadhari kwa Dr. Jogendra Nath Sahu; Dodsal Group Dar es Salaam
- Kampuni ya Milembe Co. Ltd
- Kwa yeyote anayejijua anahusika moja kwa moja au kusaidia.
Jina langu ni Askofu Charles Gadi, Mtumishi wa Mungu aliye Hai.
Kwa maovu yenu, natangaza kuwa ninyi wenyewe mmenifanya Mungu wenu na kwamba uovu wenu huu mlioufanya kwenye shamba langu sitahitaji hata msaada toka kwa Mungu kuwashughulikia, maana Neno la Mungu katika Joshua 6:26 linasema, “Amelaaniwa mbele za Bwana mtu atakayeinuka tena kujenga mji huu (Yeriko/Dorsal Group). Atakuwa ameweka msingi kwa gharama ya kufiwa na mtoto wake wa kwanza wa kiume, na ataweka malango yake gharama ya kufiwa na mwanae mdogo wa kiume.” Mungu amenipa mamlaka hii ya kuwashughulikia kiroho na kimwili watu wasiotii sheria za nchi.
Natoa masaa 72 muwe mmefunga Planti hii. Kama hamtoki ndani ya shamba langu baada ya muda uliotolewa kwisha,
- Wataalamu wote wa nje wanaofanya kazi watarudi makwao wakiwa vichaa.
- Wafanyakazi wote wanaofanya kazi hapa baada ya muda huu kuisha watakuwa ni watu wa hovyo.
- Kuhusu planti hii, baada ya muda wa saa 72 kwisha, huo mtambo hautakuwapo tena.
- Mwisho mimi nitakuwa mtu wa mwisho kutendewa uovu mkubwa namna hii na Mwenyekiti wa Dorsal Group Rajen Kilachand.
- Kwa kuwa mnaamini kuwa fedha yenu inaweza kununua kila kitu hadi haki na uhai wa mtu, hapa mmekwaa kisiki. Fedha haitawasaidia.
- Mliniahidi kwa barua kunilipa kabla ya mwezi September 2014, kabla hamjaanza kuchimba, lakini sasa mmekwenda kilomita tatu (3000m) chini ya ardhi bila ridhaa ya mwenye shamba, huku mkilala mahotelini na kufurahia wewe wafanyakazi wako. Mmesababisha uharibifu wa shamba kwa madawa na uchafu wa binadamu, mmekata miti na pia mmenizuia kwa miaka 2 kufanya maendeleo yoyote, na hadi sasa hamuonyeshi dalili zozote za kufanya mazungumzo na mwenye shamba. Ni katika nchi hii tu mnaweza kufanya hivyo si katika nchi nyingine . . . .!
- Ndani ya masaa 71 katika muda niliowapa kuna nafasi ya kufanya majadiliano lakini baada ya masaa hayo 72, si mimi wala Mungu anayeweza kubadilisha kitu.
- Mungu aliyenitambulisha Hyderabad India kwa mvua kubwa na radi tarehe 6 Juni 2015, atanitambulisha pia kwenu. Kwa habari zaidiHeavy rainfall in Hyderabad/ABN News (06-06-2015)-YouTube-http://www.youtube.com/watch?v=6Ssv6jRdmFA
- Mungu amelikuza Neno lake kuliko Jina lake lote.
Mnatakiwa muwe mmeondoka kati ya Jumanne 23 Juni hadi Alhamisi 26 Juni 2015 saa 10 jioni.
Askofu Charles Gadi
0 comments :
Post a Comment