KINANA AANZA ZIARA MKOA WA MWANZA, AKUTANA USO KWA USO NA MGOMBEA URAIS NGELEJA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa kwafuraha na Mbunge wa Jimbo la  Sengerema, ambaye pia ni mmoja wa wana CCM waliochukua fomu ya kuomba kuwania urais ndani ya chama hicho, William Ngeleja alipowasili katika Kata ya Nyamadoke, Jimbo la Buchosa,, wilayani Sengerema, kuanza ziara rasmi katika majimbo yote ya Mkoa wa Mwanza leo.

Komredi Kinana ambaye katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ameanza ziara mkoani Mwanza, baada ya kumaliza ziara katika mikoa ya Kagera na jana Mkoa wa Geita.

Akiwa mkoani Mwanza atafanya kazi ya kuimarisha uhai wa chama, kusimamia, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi  ya CCM, pamoja na kusilikiza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA; KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la  Sengerema, ambaye pia ni mmoja wa wana CCM waliochukua fomu ya kuomba kuwanua urais ndani ya chama hicho, William Ngeleja, alipowasili wilayani Sengerema.
 Chipukizi wa CCM,  akimvisha skafu Komredi Kinana wakati wa mapokezi katika Kata ya Nyamadoke, wilayani Sengerema leo.
 Komredi Kinana (kulia) akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya  katika Kata ya Nyehunge Kijiji cha Isaka, Jimbo la Buchosa, wilayaniSengerema, Mwanza leo.

 Komredi Kinana akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Bupandwa, Jimbo la Buchosa.
 Komredi Kinana akinunua ndizi na kuzigawa kwa walio kwenye msafara wake wakati wa mkutano uliofanyika katika Kijiji Bupandwa.
 Akinana mama wakishangilia kwa furaha walipokuwa wakimlaki Komredi Kinana ana msafara wake katika Kijiji cha Katwe, ambapo Komredi Kinana aliweka jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya CCM Tawi la Katwe, katika Jimbo la Buchosa, wilayani Sengerema.
 Komredi Kinana akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la msingi katika Jengo la Ofisi ya CCM Tawi la Katwe/
 Komredi Kinana akizungumza na wananchi baada ya kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Rumeya, Buchosa Wilayani Sengerema.
 Jengo lenye mashine za kusukuma maji katika Kijiji cha Rumeya, Buchosa, wilayani Sengerema.
 Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Charles Tizeba  akishngiliwa na wananchi alipowasili na Komredi Kinana katika Kijiji cha Nyakarilo, jimboni Buchosa.

 Komredi Kinana akihutubia katika Kijiji cha Nyakarilo, Jimbo la Buchosa, Sengerema.

 Wananchi wakiwa na furaha walipokuwa wakimlaki Komredi Kinana alipowasili kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Kalebezo, Kata ya Nyehunge, jimboni Buchosa.
 Komredi Kinana akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji katika Kijiji vhsa Kalebezo, Kata ya Nyehunge, Jimbo la Buchosa.
 Komredi Kinana akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akinana mama wa Kijiji cha Kalebezo, Kata ya Nyehunge, Buchosa baada ya kuzindua mradi wa maji.
 Mbunge wa Jimbo la Buchosa, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba, akielezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika jimbo la Buchosa wakati wa mkutano uliofanyika katika Kata ya Nyehunge, wilayani Sengerema.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nyehunge, Jimbo la Buchosa, wilayani Sengerama, Mwanza.
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano wa hadhara  wa CCM katika Kata ya Nyehunge, Jimbo la Buchosa.
 Komredi Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Nyehunge, Jimbo la Buchosa, wilayani Sengerama leo, ambapo aliitaka serikali na Halmashauri ya Sengerema kupunguza kwa kiasi kikubwa ushuru uliokithiri wanaotozwa wavuvi.
 Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya mti wakiwa na hamu ya kusikiliza hotuba ya Komredi Kinana wakati wa mkutano huo.

Komredfi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nyehunge, Jimbo la Buchosa, wilayani Sengerema leo, ambapo aliitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kuacha ya kuwanyanyasa wavuvi na hasa wanaotumia nyavu ndogo kuvua samaki, bali wawaadhibu wanaoagiza kutoka nje na wanaouza nchini.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment