FIFA: INTERPOL YATAKA MAAFISA 6 KUKAMATWA KWA UFISADI.

Polisi wa interpol watoa ilani ya kukamatwa kwa watu sita wanaohusishwa na FIFA

Shirika la maafisa wa polisi wa kimataifa Interpol limetoa ilani ya kukamatwa kwa watu sita wanaohusishwa na FIFA kufuatia madai ya kuhusika na ufisadi.
Agizo hilo linawalenga maafisa wanne wa mashirika makuu pamoja na maafisa wawili wakuu wa zamani wa shirikisho la soka duniani FIFA akiwemo aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Jack Warner.
Sita hao tayari walikuwa wametajwa katika mashtaka yaliofunguliwa dhidi yao na mamlaka ya mahakama za Marekani wiki iliopita.
Ilani hiyo inawalenga watu wanaotafutwa kwa lengo la kuwakamata ili wasafirishwe hadi mataifa waliohusika na ufisadi huo ili washtakiwe ,lakini mataifa hayawezi kulazimishwa kumzuilia mtu yeyote aliyetajwa.
Source BBC Swahil

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment