VIJANA WAWILI WACHOMWA KWA MOTO MPAKA KUFA KWA KUDAIWA NI WEZI.

  Watuhumiwa wakiwa wameshapigwa na kulazwa kisha kuwashiwa moto wa Matsiri, kama inavyoonekana kenye picha.
Matairi yaliyotumika kuwachomea vibaka hao yakiungua.
Matairi yakiendelea kuwaka na kuwateketeza watuhumiwa hao walituhumiwa kuwa ni vibaka.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia jinsi miili hiyo inavyoteketea.

Vijana wawili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao hawakufahamika majina yao, wanaodaiwa kuwa ni vibaka  alfajiri ya leo tarehe 23.08.214, wameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kumpora pochi dada mmoja mkazi wa Tabata Liwiti.
Shuhuda wa tukio hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema baada ya vibaka hao kumpora pochi dada huyo, walitaka kutoweka na bodaboda ndipo wananchi walifanikiwa kumkamata aliyeipora pochi hiyo akaanguka chini wakaanza kumpa kipigo huku mwenzake akifanikiwa kuondoka.
Kama waswahili wasemavyo za mwizi arobaini, kibaka huyo aliyekuwa akiendesha bodaboda kwa kasi, hakufika mbali pikipiki yake ikapata pancha naye akakamatwa na kuanza kupewa kichapo kisha walikusanywa pamoja wakavishwa matairi na kuchomwa moto.
Baada ya kuteketea kwa moto, polisi walifika eneo la tukio wakachukua mabaki ya miili ya vibaka hao na kuipeleka tatika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Source bakari ngamba blog.
(Picha/Habari na Makongoro Oging'/GPL).

Rai kutoka HABARIKA24, Wananchi tusijichukulie sheria mkononi, bali linapotokea tatizo kama hili wapelekeni watuhumiwa katika vyombo vya sheria badala ya kujichukulia sheria mkononi, pia nikosa kubwa sana.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment