BALOTELLI RASMI LIVERPOOL
Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli, 24, amekamilisha uhamisho wake kutoka AC Milan kwenda Liverpool kwa pauni milioni 16. Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City, amekubali mkataba wa muda mrefu, ingawa hakuweza kucheza dhidi ya timu yake ya zamani Jumatatu usiku.
Balotelli ambae jana tarehe 25.08.2014 alikuwa uwanjani akishuhudia jinsi timu yake mpya ya Liverpool ikifungwa magoli 3-1; aliondoka Manchester City miezi 17 iliyopita baada ya kupachika mabao 30 katika misimu mitatu.
"Uhamisho huu unawakilisha misingi ya klabu na nadhani tumefanya biashara nzuri tu hapa," amesema bosi wa Liverpool, Brendan Rodgers. Balotelli, ambaye atavaa jezi namba 45, kama inavyoonesha picha juu amesema alifanya makosa kuondoka England mwaka jana. "Nimefurahi kurejea tena, kwa sababu nilifanya makosa kuondoka England," amesema na kuongeza "Nilitaka kwenda Italy, lakini nikagundua ni makosa."
0 comments :
Post a Comment