Na Mwandishi wetu.
Wakati huu amboa modo maarufu wa Kiboongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akiwa anaendelea kusota jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga), mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki wa kizazi kipya Bongo (fleva) anaejulikana kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na polisi nchini humo.
Inasemakana alikuwa amebeba madawa tumboni na alipita vizuizi vyote mpaka alipoingia mtaani ndipo msako wa Polisi ulipomkumba na kumtia nguvuni.
Hali imekuwa mbaya sana nchini China kwa Watanzania kwani wanaishi kama Sungura, hasa hasa kwa wale wanao kwenda kwa malengo ya tofauti.
Winnie Mandela, baada ya kukamatwa na polisi.
Habari hii imetukia Habarika24 katika chumba chetu cha habari leo mchana tar 31.07.2014.
Hivyo Habarika24 inaendelea kuifuatilia kwa kina ili kuweza kujua baada ya kukamatwa nini kinaendelea, fuatailia hapa hapa tutakujuza kitakachojiri.
0 comments :
Post a Comment