MUHUJUMU UCHUMI AKAMATWA AIKOSESHA SERIKAL TSH 100 BILIONI

                                                           Na Mwandishi wetu.
Mwigulu akamata wahujumu uchumi na kubaini mtandao mchafu wa kukwepa kodi.
Katika kile kinachoaminika kuwa nikutimiza ahadi aliyoisema mhe Mwigulu wakati anaabishwa, wakati wa kuhitimisha bajeti na kwenye mkutano wa mwanza kuwa atapambana na wakwepa kodi wote na kufuta misamaha. 
Mwigulu mtoto wa mfugaji ambaye amekuwa akifananishwa na Marehemu Sokoine kwa ujasiri wake, uzalendo wake, na maadili yake amewashukia wakwepa kodi na kuwakamata handed. Leo mkurugenzi wa CI group na checknocrat wamefikishwa polisi kwa kosa la kutumia mashine feki za kutolea risiti na hivyo kukwepa kodi na kuikosesha serikali mapato. Tukio hilo limetokea leo baada ya mwigulu kiongozi anayesifika kwa "kutenda anayoyasema" kuanza rasmi vita ya kupambana na wafanyabiashara wasiowaaminifu. 
Mwigulu ambaye wabunge wa chadema walimuomba atumie mafunzo yake ya juu ya kijeshi 
(Field Marshal) kupambana na wahujumu uchumi na kwamba wanaimani naye ameridhihirisha hilo baada ya kuunasa mtandano huo mchafu ambao umeshaikosesha serikali zaidi ya 100bilion. Kampun ya CI group imekuwa ikitoa risit feki kwa makampuni ya Voda, Tigo, TBL, TCC, NMB , Seregent Beer na makampuni haya kutumia risiti feki kwenda kujichotea fedha TRA kama returns yaani marejesho tangu mwaka 2013 hadi sasa.
 Mwigulu baada ya kunasa habari hizo kwa njia zake alifika ktk ofisi hizo akiwa na polisi na kumkamata mkurugenzi wa CI group na kwenda checknocrat na kuwakamata waliotoa mashine hiyo inayotengeneza risiti feki hizo na kuagiza wawekwe lupango na wafunguliwe mashitaka ya kuhujumu uchumi.
Akiongea kwa uchungu na huruma kubwa kwa masikini Mwigulu alisema "kitendo cha wafanyabiashara wakubwa wasiowaaminifu kukwepa kodi kinasababisha Wafanyakazi kulipa kodi kubwa na kuwa na maisha magumu kwani wafanyakazi hawakwepi kodi wala hawapokei misamaha ya kodi. Mwigulu alisema mnaokwepa kodi mnawaachia mzigo wafanyakazi wakuendesha nchi kwa kodi kubwa kwenye mishahara yao midogo, mnapata huduma kwa fedha za kodi za wafanyakazi na wafanyabiashara masikini wasioweza kukwepa na hawana misamaha". Aliendelea kusema.
"Hii ni hujuma, mnasababisha masikini wakose dawa mahosipitalini, mnasababisha watoto wa masikini wakose fedha za mikopo ya elimu ya juu, mnasababisha watoto wa masikini wakose elimu bora, mnasababisha watanzania wakose maji. Ninyi mnafanya biashara na kupata huduma kwa kodi za masikini, tunatengeneza pengo. la walionacho, ninyi wachache mnaokwepa kodi na kundi la masikini wasionacho wanaobeba mzigo wa kulipa kodi. Hii ni hujuma dhidi ya uchumi wa Tanzania niliyoapa kupambana nayo".
Watu walifurika maeneo ya pembezoni mwa matukio yote mawili huku mmoja akisikika na kusema naona Sokoine amefufuka, hawa watu wamezoea kukwepa kodi waziwazi na kutoa rushwa na wanajulikana ila hakukuwa na jasiri wa kuwakamata. Sasa mwanaume huyu akisema anatenda kwa ujasiri. 
Mwingine akasikika akisema Mwigulu ndio habari ya mjini kwa sasa, vijiwen na sokoni wanasema ndiye Rais wa 2015 kwakuwa ndiye anayejali masikini, anajua maisha ya masikini, aajua njia ya kumwinua masikini na anafanya kwa vitendo bila uoga. Mwingine akasikika akisema huyu CCM wakimsimamisha Urais 2015 waashinda saa nne asubuhi tu.

                                                             Mkurugenzi wa CI group.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment