UJAMBAZI WATOKEA ARUSHA.

Arusha jana tarehe 22.08.2014, saa majira ya tano usiku, ndugu yetu pichani (jina hatujabahatika kulipata) akiwa na familia yake ya watoto wawili wa kike alitoka dinner, walipokuwa wanarudi nyumbani mara walitokea watu wawili wakiwa kwenye toyo wakasimamisha gari yao na kuwaamuru watoe vyote walivyonavyo, kaka akawasha gari na kukimbia.
Baba wa marehem akiwa na wanawe. 

Na Joyce Kiria Page.
 Wale watu wa toyo nao wakaanza kuwafuata, wakaanza kukimbizana wakiwa wanaelekea mbauda ndipo watu waliokua kwenye toyo wakaamua kupiga risasi kwa nyuma!

 Kwabahati mbaya ikampata mtoto wake wa miaka nane ambae alikuwa amelala kwenye siti ya nyuma straight kwenye ubongo, lakini wazazi wale waliendelea kuendesha gari hawakuweza kufahamu kwa haraka kama risasi iliyopigwa ilipenya na kumpiga mwanae,  walipofika mahala penye usalama wakaamua kuangalia ni nini kilichojiri, ndio wanaona mtoto damu zinamtoka machoni ikabidi wamkimbize hospitali ya Mount meru lakini walishindwa kumtoa risasi na mtoto akafariki majira ya saa saba usiku huo huo!!!
Baba wa mtoto anafanya kazi UN nchini Liberia alirudi  likizo na kutokana na hili tatizo la ugonjwa wa Ebola,
                      Mtoto aliye uwawa kwa risasi na majamabazi walio kuwa kwenye toyo.
                                                 Picha zote kwa hisana ya Salma Mvungi.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment