NAIBU WAZIRI FEDHA MH. MWIGULU NCHEMA AIFAGILIA UTT MICROFINANCE.

 Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Taasisi ya kifedha ya UTT Microfinance, baada ya kukata utepe kuzindua taasisi hiyo, Dar es Salaam jana.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto), akikata utepe kuzindua rasmi Taasisi ya huduma za Kifedha ya UTT Microfinance, Dar es Salaam jana. Wa pili Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Balozi Fadhili Mbaga na Mtendaji Mkuu wa UTT, Bw. James Washima (kushoto).
Naibu Waziri wa Fedha Bw. Mwigulu Nchemba (katikati), akimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kifedha ya UTT Microfinance, Bw. James Washima wakati akimuonyesha vipeperushi, Dar es Salaam jana.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Fadhil Mbaga.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kifedha ya UTT Balozi Fadhil Mbaga (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bw. James Washima wakimwangalia Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba.


Naibu Waziri Fedha aifagilia UTT Microfinance

NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali imevutiwa na utendaji kazi mzuri wa Taaisisi ya kifedha ya UTT Microfinance kuwa na matawi 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa muda mfupi.

Akizungumza wakati wa kukata utepe kuzindua rasmi Taasisi hiyo Sukari House Dar es Salaam jana, Naibu Waziri amesema, Serikali imefurahishwa na dhamira ya kweli ya kufikisha huduma za kifedha karibu na wananchi kila pembe ya nchi kunakofanywa na UTT.

“Hii inaonyesha, mmeshaanza kutoa aina nane ya huduma kama mikopo, uwakala wa Bima, Uwakala wa Benki, uwakala  mkuu wa mitandao ya simu (mobile money super agent) kwa mwaka mmoja tangu kuanzishwa”.

Bw. Nchemba amesema, kazi kubwa iliyoifanya ndani ya muda mfupi na kuwa na matawi 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi yameifurahisha na kuahidi kuwa Serikali itatoa ushirikiano wa karibu kwa taasisi hiyo ili iweze kufikia malengo iliyokusudia.

Naibu Waziri amebainisha kuwa uwa serikali iliamua kwa makusudi kuanzisha taasisi hiyo ili kuwezesha wananchi kiuchumii hususan wenye miradi, kama biashara ndogondogo na za kati ambao wamekuwa wakipata changamoto nyingi katika kupata mikopo na huduma nyingine za kifedha toka taasisi kubwa za kifedha na  mabenki ya biashara ambayo mara nyingi muundo na mfumo wa taasisi hizo huambatana na masharti magumu.

“Wengi walishindwa kupata mikopo stahiki kutokana na masharti, hususani wenye vipato vya chini, sharti la dhamana ya mali isiyo hamishika kama nyumba, kiwanja na mali, ambavyo hawana”, anasema Bw. Nchemba na kusisitiza kuwa Serikali imeanzisha UTT Microfinance kuchochea ukuaji wa uchumi na kuwainua watanzania walio wengi.

Awali kabla ya uzinduzi huo, UTT Microfinance imezindua rasmi mtandao wa matawi sehemu mbalimbali nchini kwa lengo la kufikisha huduma za kifedha karibu na wananchi hususan mikopo nafuu kwa wajasiriamaliri ambapo matawi 10 yaliyopo katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Zanzibar ulizinduliwa rasmi katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, wakurugenzi wa mashirika, Makampuni na Taasisi mbalimbali pamoja na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Mweneykiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTT MFI Balozi Fadhili Mbaga, alisema watahakikisha kuwa UTT MFI inatekeleza azma yake kwa ufanisi na pia itashirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali.

“Tunapenda kusisitiza dhamira yetu ya kuendelea kushirikaiana na wadau mbalimbali hususan Tanzania Microfinance Association katika jitihada za jumla za kuwa na mfumo mzuri wa huduma za kifedha na mitaji midogo na kuhakikisha kuwa huduma hizi zinawafikia watanzania wengi zaidi na kuwa chachu muhimu ya maendeleo ya jamii yetu”, anasema Balozi Mbaga.

Ameishukuru serikali kwa ushirikiano inayotoa kwa taasisi hiyo na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizo mbele yao kuhakikisha wanavuka malengo waliyojiwekea. ameiomba serekali isisite kuwaunganisha na wabia na washirika mbalimbali ili kuwa na mtandao mpana zaidi wenye nguvu ya kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa UTT MFI James Washima, alisema wanaamini Serikali haikufanya makosa hata kidogo katika kuanzisha UTT MFI, akiahidi kututumia uzoefu wao wa mwaka mmoja, ambao umebaini kuwa huduma za kifedha na mikopo hususan kwa wajasiriamali na watanzania wa kada za kati na chini zilisubiriwa kwa hamu kubwa sana.

Bw. Washima amesema kiu ya Watanzania kwa huduma za UTT hivyo taasisi yao imejipanga kutoa huduma nzuri. Ameahidi kuwa ndani ya miezi sita wataongeza idadi ya wafanyakazi kwani waliopo ni wachache ambapo mfanyakazi mmoja anahudumia wateja zaini ya 1,000.

 “Huu ni muitikio mzuri kutoka kwa jamii na sisi tunajitahidi kukabiliana nao kwa ufanisi” anabainisha Bw. Washima na kuongeza kuwa hivi sasa wana matawi 10,  manne yakiwa Dare s Salaam - Sukari House, Azikiwe, Kijitonyama na Chang’ombe.

Bw. Washima anayataja matawi mengine kuwa ni Arusha lililopo Ngarenaro, Meru lililopo Jengo la Posta Meru,  Dodoma lililopo Posta Dodoma, Mbeya barabara ya KKKT, Mwanza katika jengo la Posta na Zanzibar, Jengo la Posta Kijangwani.

Akizungumzia m,afanikio ndani ya mwaka mmoja wa uwepo wao, Bw. Washima anasema wameweza kukuza mtaji wa Taasisi toka  Shilingi billion 5.4 mnamo Julai mwaka 2013 na kufikia bilioni 12  Juni, 2014. Pia taasisi imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Tsh 5.316 bilioni, kwa wakopaji 6,102 – huku 84% ya wakopaji wote wakiwa ni wanawake.

Anabainisha kuwa pia wameanzisha huduma za moja kwa moja kwa muhusika (Tailor-made) kama vile mikopo kwa ajili ya Bima ya matibabu, Hati Malipo (Contract Financing loans), mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wadogo wadogo (Group loans), Mikopo kwa ajili ya SACCOS, Mikopo maalumu kwa miradi inayolenga kuongeza thamani ya bidhaa na ajira ikiwemo viwanda vidogo vidogo, mikopo kwa wafanyakazi wa Serikali. 

Hata hivyo, pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana, Washima alieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwa kuibuka kwa taasisi na kampuni zisizo rasmi ambazo hutoa huduma za kifedha hususan mikopo kwa watu wa kada za chini.

Mtendaji huyo amesema mengi ya makampuni haya mara huwa ya kilaghai na yenye kuchukua riba kubwa bila utaratibu maalum suala ambalo badala ya kuwasaidia watu, huwaumiza na kuwaua kabisa kiuchumi.

“Tunaiomba serikali iharakishe utungwaji wa sera ya kurasimisha huduma hizi ili zifanywe kwa utaratibu maalum na pia ziratibiwe na kudhibitiwa vizuri ili wananchi wasiendelee kutaabika na kufilisiwa na watu wasio na nia njema ambao hutumia fursa ya udhaifu wa kisera kujinufaisha” alisema Washima.

UTT MFI ni Taasisi ya huduma za fedha na mikopo iliyoanzishwa mnamo Juni 2013 kwa lengo la kutekeleza sera za serikali katika uwezeshaji kiuchumi hususan kwa wajarisiamali, watumishi wa umma, wakulima, wenye viwanda vidogo, watu wasio na ajira rasmi na wananchi wote kwa ujumla.



UTT MFI pia inalenga kuwapa fursa wamiliki wa Vipande vya UTT AMIS kutumia vipande vyao kama dhamana wakati wa kuchukua mikopo, kupanua wigo na kurahisisha uwekezaji wa vipande vya UTT na hivyo kukuza utamaduni wa kuwekeza kwa wananchi.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment