Na mwandishi wetu mtaani
Kibonde wa Clouds anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, amemgonga dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walipofika kupima ajali, Kibonde karudi nyuma kaendesha gari lake na kukimbia! Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia.
Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge. Trafiki aliingia ktk gari lake nakumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde kagoma na kumtaka trafiki ashuke ktk gari lake, trafiki naye kagoma kushuka.
Mchezo ulioendelea Kibonde aliondoa gari na kuanza kupiga misele, akizunguka mitaa akiwa na trafiki huyo! Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kila kiunga cha jiji hususani eneo la Mwenge na Ubungo.
Hatiye, Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo shuhuda wetu akashuhudia senema ya Kibonde na trafiki! Trafiki wa kike aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde iliyokuwa kasi, gari hiyo haikuonesha dalili za kupunguza mwendo.
Trafiki alikomaa kusimama mkono wake ukiwa juu kuashiria kumtaka Kibonde asimame huku akipaza sauti ktk radio call akisema "ananigonga afande, ananigongaa"!
Akiwa ktk hali hiyo, kuna gari ilikotokea sikujua ikakatisha kati ya trafiki na gari ya Kibonde ndiyo ikawa kigingi cha gari ya Kibonde na kutiwa mbaroni!
Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki ambapo kwa sasa amepelekwa Oystabay! Kwa utafiti kidogo nilioufanya nikifukuzana na muda, ni kwamba Kibonde na watu wengine aliokuwanao ndani ya gari lake walikuwa 'WAMELEWA'!
Kibonde akikabiliana na Trafiki.
Kibonde akiwa maabusu
0 comments :
Post a Comment