Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa ya utatuzi wa migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.
Wanahabari wakiwa katika mkutano na Bwana Makonda.
Waandishi wa habari kutoka vyombombalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema atachukua sehemu ya mshahara wake kwa ajili ya kuwalipa wanasheria watano watakao kuwa wanafanya kazi ya kusikiliza na kuwasaidia wananchi wenye migogoro ya ardhi.
Makonda alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utatuzi wa migogoro ya ardhi katika wilaya yake ya Kinondoni Dar es Salaam leo asubuhi.
"Kama nilivyobadilisha mfumo mzima wa PF3 ndivyo ninavyofanya kwenye ardhi nimechukua hatua mahususi kuchukua sehemu ya mshahara wangu na kuajiri jumla ya wanasheria watano watakao wasaidia wananchi hasa wanyonge kupata haki zao juu ya madai yao mbalimbali yahusuyo ardhi" alisema Makonda.
Alisema wanasheria hao watachukua asilimia 75 ya mshahara wake kwa kazi hiyo hivyo mwananchi wa Wilaya ya Kinondoni hatatakiwa kulipa hata senti tano atakapokuwa amekwenda kupata huduma hiyo.
Makonda alisema kuwa kuanzia Jumatatu ya Juni 15, 2015 wanasheria hao watakuwepo ofini kwake watakaofanya kazi saa zote kwa lengo la kusaidia ili wapate uelewa wa kisheria juu ya haki zao zozote kuhusu umiliki wa ardhi.
Makonda alisema heshima aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete ya kumteua kuwa mkuu wa wilaya hiyo kwake anatafsiri kama changamoto kubwa ya kuhakikisha anashughulikia kwa kina matatizo ya msingi ya wilaya hiyo.
Alisema katika wakati huu huwezi kutaja changamoto kubwa tatu za wilaya hiyo ukaacha kutaja migogoro ya ardhi na kuwa kwa ufafanuzi zaidi unaweza kurejea hotuba yake ya Februari 28, 2015 wakati akianza kazi mambo aliyoyataja na kuyapa kipaumbele ambapo alitenga kila siku ya Ijumaa kuwa ni siku ya kukutana na watu wenye migogoro ya ardhi ili kuitatua.
Makonda alisema ili kumaliza changamoto hiyo ya migogoro ya ardhi kama si kuipunguza kwa kiwango cha juu kila mkazi wa wilaya hiyo anatakiwa kuchukua kopi ya hati au nyaraka yoyote ile inayompa uhalali wa kumiliki ardhi, shamba au kiwanja na kopi hizo zipelekwe kwa ofisi ya mtendaji wa kata kwani kuanzia Julai 2, 2015 yeye na timu ya watu wa ardhi atahamishia ofisi yake kwenye kata hizo kwa ajili ya kuzihakiki nyaraka hizo.
Alisema pindi watakapo baini kuwa kiwanja kimoja kina zaidi ya mmiliki mmoja watamtafuta mmiliki halali kupitia vyombo walivyonavyo na atakayebainika ameghusi atachuliwa hatua.
Alisema lengo la kuhamishia ofisi yake kwenye kata ni kufuta kabisa uzoefu wa kusikitisha wa wananchi mmoja kugundua kwamba kiwanja chake kinamilikiwa na mtu mwingine baada ya kumwaga roli la mchanga ama tofali. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com- simu namba 0712-727062)
0 comments :
Post a Comment