MAELFU ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM, na wakazi wengine wa jiji la Mwanza, leo Ijumaa Juni 5, 2015, walifurika kwa wingi kwenye ofisi za CCM wilaya ya Nayamagana na ile ya Ilemela, wengine wakitaka kumuona na kupeana mikono na wengine kwa nia ya kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edwrad Lowassa, alipofika jijini Mwanza kutafuta wana CCM wa kumdhamini katika safari yake ya Matumaini. (Kuwania urais wa Tanzania kupitia CCM).
Madereva texi, waendesha bodaboda, na hata wafanyakazi na wasafiri kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, waliacha shughuli zao kwa muda ili walau wamuone mtangaza nia huyo wa nafasi ya jurasi kupitia CCM.
Lowassa alichukua fomu, za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania, Alhamisi Juni 4, 2015 pale makao makuu ya CCM, na safari yake ya kusaka wadhamini ilianza “chap chap” pale pale Dodoma, na Mwanza ndio kituo cha kwanza nje ya Dodoma, ambacho Lowassa, ameanza kampeni yake ya kusaka wadhamini.
Picha ni, Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, ambaye tayari amechukua fomu za kuomba CCM imteue kuwania urais, Edwrad Lowassa, akipungia mkono maelfu ya wanachama wa chama hicho na wananchi wengine baada ya kupata wadhamini kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Ijumaa Juni 5, 2015. (Picha na K-VIS MEDIA) |
0 comments :
Post a Comment