KAMPUNI YA MASOKO, NEC, OSIEA PAMOJA NA WASANII WAZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA UPIGAJI KURA

 Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko, Conctantine Magavila (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuhamasisha vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na hatimaye kupiga kura ilijulikanayo kama 'Kuradili". Kampuni hiyo itafanya kampeni hiyo katika mikoa kadhaa kwa kushiriakiana na  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Shirika la Open Society International East Africa (OSIEA), pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki. Kulia ni mwanamuziki Sinura Mushi na kushoto ni Ofisa Elimu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rose Malo. 
  Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko, Conctantine Magavila (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwanamuziki Stamina, Kala Jeremia, Snura, Ofisa Elimu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rose Malo na Ofisa Mipango Msaidizi wa Shirika la Open Society International East Africa (OSIEA), Adam Anthony.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanamuziki wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni  Stamina, Kala Jeremia, na Snura
Wanamuziki hao wakiimba wimbo maalumu walioutunga wa kuhamasisha kupiga kura kupitia kampeni yao ya KURAdili mbele ya wanahabari.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI  ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na  shirika la Open Society International East Africa (OSIEA) na wasanii mbalimbali wa muziki wamezindua  kampeni maalumu ya kuwahamasisha vijana
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na hatimaye kupiga kura.


Kampeni hiyo iliyozinduliwa Jijini Dar es Salaam leo  inatarajiwa
kuhusisha mikoa mitano ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza,Shinyanga na Morogoro ambapo yatafanyika matamasha mbalimbali ambayo hayana viingilio  na yatakayowahusisha wasanii walioteuliwa kama
mabalozi katika kampeni hii.


Kauli mbiu ya kampeni hii ni ‘Kura dili’ na lengo kuu ni kuhakikisha vijana wengi iwezekanavyo wanajiandikisha na kujitokeza kwa wingi kupiga kura.


Wasanii watano wametunga wimbo maalumu uitwao ‘Kuradili ambao pia ulizinduliwa katika hafla hiyo na utatumika katika kampeni hii.


Wasanii hao ni pamoja na Gnako, Snura, Izo Biznez, Kala Jeremiah na Stamina.


Akizungumza kwa niaba ya Masoko,mmoja wa wakurugenzi, Constantine Magavila alisema kampeni hiyo inalenga kuwafikia zaidi ya watu milioni 4 kujisajili na kupiga kura na watashirikiana na redio mbalimbali kuhakikisha wimbo huo maalumu unapigwa katika redio mbalimbali ili
kuhamasisha zaidi.


“Tumegudua kuwa vijana wanaweza kuleta mabadiliko makubwa sana endapo watajitokeza kupiga kura kwa wingi kwa hivyo tunaanza kwanza kuwahamasisha wajitokeze kupiga kura na baadaye waende kupiga kura kwa
wingi,” alisema.


Alisema kampeni hii itahusisha mikoa mitano lakini wanaamini ujumbe utasambaa Tanzania nzima ili vijana waweze kutambiua kuwa kura ni dili kama kauli mbiu ya kampeni hiyo inavyosema.


“Tunaamini kampeni hii itakuwa na mafanikio makubwa na uchaguzi wa mwaka huu utavunja rekodi,” alisema na kuongeza kuwa watashirikiana na NEC kuhakikisha hili linafanyika.


Naye mwakilishi wa OSIEA ambaye ni Meneja Mkazi, Agnes Hunt, ambaye shirika lake lilisaidia katika kurekodi wimbo huo maalumu alisema kuwa wanashirikiana na mashirika mbalimbali yakiwemo yasiyo ya kiserikali katika masuala ya uwazi na utawala bora.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Elimu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kitaifa, Rose Malo aliishukuru Kampuni ya Masoko kwa jitihada zake za kuhamasisha vijana na kusema kuwa NEC haina fedha za kutosha hivi
inategemea makampuni kama haya kujitokeza na kusaidia wakati kama huu.


Alisema Masoko imepewa kibali ya kutoa elimu ya upigaji kura ikiwemo uandikishaji katika daftari la wapiga kura.
“Unaweza kuhamasisha vijana kujiandikisha na wakafanya hivyo lakini wakaacha kujitokeza siku ya kupiga kura…hii itakuwa kazi bure kwa hivyo kampeni hii itasaidia kuwafikia hawa vijana na kuwahamasisha wajiandikishe na pia wajitokeze kupiga kura,” alisema na kuwapongeza
wasanii wote walioshiriki katika jitihada hii.


Izo Biznez ambaye ni mmoja wa wasanii watakaoshiriki katika kampeni hiyo alisema, “Sisi kama wasanii tunashukuru kupata nafasi kama hii ya kuongeana vijana na kuwahamasisha wajiokeze kujiandikisha na kupiga kura ifikapo mwezi Oktoba 25 mwaka huu.” 
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com-simu namba 0712-727062)

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment