Waziri wa Wizara ya Sayansi pro. Makame Mbawara akielezea Data Center iliyojengwa hapa Tanzania kwa waandishi wa habari. Pembeni yake ni Director wa ICT Dr. Ally Simba.
Mr. Jiang Xin (Product Manager wa Huawei Enterprises) akielezea Data Center.
.................................................................………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya Huawei Tanzania ikishirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wameandaa kongamano la kwanza la sekta ya TEHAMA (ICT) ijulikanayo kama Huawei Cloud Conference kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC).
Kongamano hili liliwakutanisha wadau wote wa TEHAMA (ICT) nchini, wakiwemo wa serikali na wa sekta binafsi na lilizinduliwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lv Youquin, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Patrick Makungu pamoja na usimamizi wa makampuni shirika ya Huawei Tanzania kutoka; Airtel, Viettel, Tigo, Vodacom, na TTCL.
Katika Kongamano hilo la mada “Rahisisha Teknolojia, Rahisisha Biashara” ilizungumziwa hali ya sasa ya sekta ya TEHAMA, sera zake pamoja na kupanga jinsi ya kuiendeleza sekta hii nchini ili kufikia malengo ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ya millenia ya 2025 ambayo ni kuendeleza Tanzania kupitia TEHAMA.
Katika kongamano hili kampuni ya Huawei Tanzania (ambao ni wabunifu wakubwa wa bidhaa na huduma za TEHAMA) pamoja na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia walitia sahihi mkataba wa makubaliano kati yao huku ikiipa nafasi kampuni ya Huawei Tanzania kua moja ya washauri wa mambo ya TEHAMA nchini.
Baada ya kutia sahihi, Kampuni ya Huawei Tanzania ilielezea mipango yake ya kuendeleza na kukuza mawasiliano nchini Tanzania kwa kukuza sekta ya TEHAMA na kutoa elimu serikalini, mashuleni na kwa wananchi wote kwa ujumla kuhusu sekta iyo.
Tanzania imekua ikifanya kazi kwa karibu sana na Kampuni ya Huawei Tanzania na kwa mda wote kampuni hii imeshirikiana na wizara kwa karibu sana. Utiaji sahihi wa makubaliano ya kushirikiana katika shughuli za TEHAMA ni ushuhuda tosha wa jinsi Huawei Tanzania inavyojali sekta ya TEHAMA nchini na itaendeleza kukuza teknolojia hiyo nchini.
Tanzania imekua ikifanya kazi kwa karibu sana na Kampuni ya Huawei Tanzania na kwa mda wote kampuni hii imeshirikiana na wizara kwa karibu sana. Utiaji sahihi wa makubaliano ya kushirikiana katika shughuli za TEHAMA ni ushuhuda tosha wa jinsi Huawei Tanzania inavyojali sekta ya TEHAMA nchini na itaendeleza kukuza teknolojia hiyo nchini.
Akizungumza katika Kongamano hilo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technolojia, Prof. Makame Mbarawa alisema, “TEHAMA inachangia sana katika maendeleo ya Uchumi ya nchi kwani inawezesha mambo kufanyika kwa ufanisi zaidi. Wizara na serikali kwa ujumla imekuwa na mahusinao mazuri na Kampuni ya Huawei Tanzania, na tumesha shirikiana katika miradi mingi.
Pamoja na ubunifu wake katika sekta ya TEHAMA, Huawei imechangia sana katika mambo mbali mbali nchini Tanzania. Kufikia kwenye Mkataba wa Makubaliano kati ya Wizara na Huawei ni ishara ya ubora wa kazi ambayo kampuni hii, na itaendeleza ubadilishinaji wa teknolojia kati ya Huawei na Tanzania. Huawei imechangia pakubwa katika ukuaji wa sekta ya TEHAMA nchini Tanzania.
Naye Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lv Youquin alisema, “ Kwa mda mrefu Tanzania na China wamekua na mahusiano mazuri hususan baada ya ujio wa raisi wa china bwa. Xi Jinping mwaka 2013; Kampuni nyingi za kichina zimekuja Tanzania kuwekeza na kukuza nchi.
Kama kiongozi wa mambo ya TEHAMA duniani, Huawei imewekeza nchini Tanzania kwa Zaidi ya miaka 17 na kwa muda wote huo imetoa ajira nyingi kwa watanzania pamoja na kuwekeza kwenye shughuli za kijamii nchini, na kuwa mfani wa kuiga katika maswala ya kidiplomasia kati ya Tanzania na China.
Katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Patrick J Makingu aliwapongeza Huawei kwa mchango wao katika kujenga Tanzania bora kupitia TEHAMA na kuwasihi makampuni mengine ya TEHAMA kuiga mfano wa Huawei.
Aliendelea kwa kusema, “Huawei imekuwa ikijikita katika kutafuta suluhisho mpya katika sekta ya TEHAMA duniani. Awali mwaka huu, Huawei ilihusika katika Kongamano la Mobile World Congress mjini Barcelona nchini Uhispania ambapo walikuwa moja kati ya mashirika makubwa kufanya maonyesho ya bidhaa zake mpya na sisi kama Wizara tunajivunia kufanya kazi nao”.
Naye Mtendaji Mkuu wa Huawei Tanzania Bw. Zhang Yongquan alisema “Kampuni ya Huawei Tanzania imekuwepo nchini kwa takribani miaka 17 na imejishughulisha katika shughuli mbalimbali za kujenga nchi ikiwepo shughuli za kijamii hususani kwenye michango vyuoni na mahospitalini. Bw. Zhang Yongquan, aliendelea kwa kusema “Tunashukuru serikali ya Tanzania pamoja na wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa kuendelea kuiunga mkono kampuni yetu”.
Katika kongamano hilo, kampuni ya Huawei Tanzania ilizindua bidhaa zake mpya Oceanstor V3 and Fusioncube. Pia imeonyesha Truck yao inayozunguka nchi mbalimbali kila mara moja kwa mwaka ikianzania nchini China, na kwa mwaka huu truck hili linazunguka kusini na magharibi mwa bara la Afrika.
Kampuni ya Huawei Tanzania inaongoza katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Tanzania na imekua ikishirikiana na wadau wengine wa mawasiliano kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel na TTCL katika kuchangia ukuaji wa watu binafsi kwenye hii sekta (ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).
0 comments :
Post a Comment