WAKALA WA USAJILI UFILISI NA UDHAMINI (RITA) YASAJILI NA KUTOA VYETI 5,081 KWA SHULE ZOTE ZA WILAYA YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

 Msajili wa Vizazi na Vifo wa Wilaya ya Kinondoni, Mariam Ling'ande (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu maendeleo ya kampeni ya usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa wanafunzi wa shule za msingi katika Wilaya ya Kinondoni. Kushoto ni Meneja Masoko Mawasiliano Elimu kwa Umma wa  Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Josephat Kimaro.
 Meneja Masoko Mawasiliano Elimu kwa Umma wa  Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Josephat Kimaro (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita) umesajili na kutoa vyeti  5,081 katika shule zote zilizopo wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano na Masoko wa wakala hao Josephat Kimaro wakati akitoa majumuisho ya kampeni ya kusajili na kuwapa vyeti vya kuzaliwa wanafunzi wote walio katika shule za msingi za Kinondoni.

Alisema kati ya wanafunzi hao waliosajiliwa wasichana 2,720 na wasichana 2,361  na katika idadi hiyo wanafunzi waliopatiwa vyeti ni katika shule 56 ambapo katika wilaya hiyo ina jumla ya shule 140.

Alisema kampeni hiyo ni muendelezo wa mkakati uliozinduliwa katika manispaa ya Ilala na jumla ya wanafunzi 16,200 walishasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.

"Ni vyema wazazi na walezi walio na watoto wanaosoma katika shule za msingi na manispaa ya Kinondoni kutumia fursa hii kuwapatia watoto wao vyeti vya kuzaliwa,"alisema.

Wakati huo huo Msajili wa Vizazi na Vifo katika wilaya hiyo Mariamu
Ling'ande  alisema wao huwa wanatoa vyeti kwa wale wote ambao wanazaliwa katika ardhi ya Tanzania Bara.

"Kuna malalamiko watu wanayodai kuwa  ofisi yetu inatoa tu vyeti lakini suala hilo si la kweli kabisa na ni ukweli kuwa vyeti vya kuzaliwa  mtu anapata pale ambapo amezaliwa haijalishi ni wa nchi gani,"alisema.

Alisema katika kutoa vyeti hivyo kuna kila aina ya vigezo huwa wanaviangalia ili kuthibitisha kuwa mtu huyo ni kweli ni mtanzania na pia ni kweli alizaliwa katika ardhi ya Tanzania Bara.
 

(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment