UNESCO WATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU WA VYUO VYA UALIMU HAPA NCHINI

Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo ya matumizi ya Tehama katika ufundishaji kwenye vyuo vya ualimu.
.........................................................................................................................
Na Geofrey Adroph, Pamoja blog.

  Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu ya Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limejikita katika uboreshaji wa elimu kwa kuwapa mafunzo walimu katika somo la Teknnolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Akizungumza leo katika Ufungaji wa Mafunzo yaliyoandaliwa na UNESCO wakishirikiana na China Funds in Trust Project (CFIT) yaliyofanyika kwa siku tano katika Ukumbi wa DIT, Jijini Dar es Salaam, Ofisa Miradi wa UNESCO, Faith Shayo amesema mafunzo waliopata walimu wa vyuo vya walimu mbalimbali nchini itawasaidia katika uboresha wa elimu ikiwa ni pamoja na kuwapa vifaa vitakavyotumika katika kufundishia somo hilo.

Faith amesema ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya Tehama hii inatokana na baada ya mkutano wa viongozi wa vyuo mbalimbali pamoja na wadau wa elimu wa hapa nchini kuona kuna mapungufu katika masuala la uelewa na matumizi ya Tehama katika vyuo vilivyopo nchini. Amesema katika kufikia malengo ya mradi wa UNESCO-China Funds in Trust Project (CFIT) wanaoshirikiana na vyuo vya elimu hapa nchini kwa malengo makuu matatu.

  Aliyataja malengo hayo ni kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya ualimu, kuweka mafunzo ya walimu wanapofundisha katika somo la Tehama ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuwanunulia vifaa vya Tehama ambavyo vitasaidia katika kufundishia. Faith amesema baada ya mafunzo hayo vyuo vitapata vifaa mbalimbali ambayo ni kompyuta, Projecta,ya na vifaa vya kuzalisha umeme wa jua (Solar Energy) kwa ajili ya kuondokana na tatizo umeme unaokatika katika mara kwa mara.

  Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara kutoka (DIT), Daudi Mboma pamoja na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Godfrey Haongo ambao wanajukumu la kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo tofauti hapa . Waliopata mafunzo hayo Waalimu tisa wa Chuo cha Ualimu Tabora, na tisa wengine kutoka chuo cha ualimu Monduli , walimu wanne kutoka chuo cha ualimu Morogoro, na mmoja kutoka Shule direct, wawili kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso District.

  Mafunzo hayo yametolewa kwa baadhi ya watumishi wa Wizara ya elimu ambao wana mchango mkubwa hasa katika ukuzaji wa Tehama wakishirikiana na wanafanya kazi wa UNESCO ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo kwa vyuo vya elimu hapa nchini.

 Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya Tehama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa mafunzo ya kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa huduma za kitehama katika taifa kwa kuanzisha mradi huo wa kutoa mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo katika ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo mkubwa wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika kufanya nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment