NYOTA YA LOWASSA YAZIDI KUNG'ARA AWAPIKU WENZAKE KWA ASILIMIA 20 NI KATIKA KUWANIA URAIS WA TANZANIA

Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Samunge Social Research Centre, George Nyaronga kutoka Chuo Kikuu Huria (OUT).
Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Samunge Social Research Centre, George Nyaronga (katikati), akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kuhusu viongozi wanaotaka kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu ambapo Waziri Mkuu wa zamani,  Edward Lowassa ameonesha kuwapiku wenzake kwa kupata asilimia 20 akifuatiwa na  Dk.Willibrod Slaa aliyepata asilimia 11.7. Kushoto ni Mtafiti Msaidizi wa utafiti huo, Wakili Mambo na kulia ni Mtafiti Msaidizi wa utafiti huo, Gideon Anyona kutoka Chuo Kikuu cha Kenyata.

 Wanahabari wakisubiri kuchukua taarifa hiyo.

Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

NYOTA ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa yazidi kung'aa baada utafiti uliofanywa na Samunge Social Research Center na kugundua wananchi wengi kumpenda na kumuhitaji agombea urais wa mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi Mtafiti Mkuu wa Tafiti  hiyo George Nyaronga alisema baada ya Waziri huyo kudai kuwa atagombania wananchi wengi wameonyesha kumuhitaji kwa kiasi kikubwa.

Alisema katika utafiti huo walioufanya waligundua kuwa Waziri huyo mstaafu anaongoza kwa asilimia nyingi kuliko wenzake anaowafata.

Akitaja asilimia hizo alisema Edward Lowassa anaongoza kwa asilimia 20.7 akifuatiwa na Wilbroad Slaa asilimia 11.7, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (Chadema)Freeman Mbowe asilimia 3.4, Mwenyekiti wa Chama cha Wanachi CUF Ibrahim Lipumba asilimia 4.2.

Wengine ni pamoja na Waziri wa Ujenzi John Magufuli 7.6, Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba asilimia 4,Waziri Mkuu Mizengo Pinda asilimia 2.4,Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Bernard Membe7.0 na Mwenyekiti wa chama cha Nccr Mageuzi James Mbatia 1.2.

Alisema kwa kutokana na nchi kuelekea katika uchaguzi wananchi wamekuwa na muamko wa hali ya juu katika kuhakikisha kila mmoja atapigapiga kura kwa mwaka huu.

"Tumefanya tafiti hizi na kuona kwamba watanzania wengi wameamua kuingia kwenye masuala ya siasa na kuleta mabadiliko katika nchi yao na si kupigiwa kura,"alisema.

Alisema kutokana na utafiti wao wamegundua kuwa wananchi wanahitaji rais ambaye ni muadilifu, msema ukweli, mwenye afya asiwe na udini wala ukabila na mzalendo wa nchi yake

Alisema kutokana na majina hayo ya urais pia katika tafiti zao imeonekana kuwa vyama vinavyoongoza katika kupendwa na wananchi ni pamoja na Chama cha Mapinduzi kuonekana kupendwa sana kuliko vyama vyote.

Alivitaja vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) 53.5,Chama cha Demokrasia (Chadema) 34.2 ,Chama cha Wazalendo (ACT)1.2 na Umoja wa Katiba Mpya (Ukawa) 6 na Chama cha wanachi CUF 6. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment