JUMA NATURE NA WENZAKE KUITEKA DAR ES SALAAM KATIKA TAMASHA LA KOMAA LITAKALOFANYIKA JUMAMOSI UKUMBI WA DAR LIVE MBAGALA

Msanii Juma Nature 'Kiroboto' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la kuadhimisha miaka 16 ya kazi zake za muziki nchini  pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za Kituo cha Redio cha EFM linalofahamika kwa jina la Komaa Concert litakalofanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi Ukumbi wa Dar Live Mbagala kuanzia saa 12 jioni. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo, ambao ni waandaaji wa tamasha hilo. Kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Msanii Said Christopher 'Mucky), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha hilo,Msanii  Juma Nature, Msanii, Semani Jabiri 'Msagasumu' na Msanii Snura Mushi.
Wasanii watakaotoa burudani la nguvu siku hiyo ya tamasha. Kutoka kulia, Fredy Felix 'Fredwayne' Juma Nature, Snura Mushia, na Said Christopher 'Mucky)
Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Lydia Moyo (kushoto), akiperuzi simu yake katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.

............................................................................................................
                              TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                                              KOMAA CONCERT

Tamasha kubwa la kuadhimisha miaka kumi na sita ya msanii JUMA NATURE  maarufu kama kiroboto pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika kama KOMAA CONCERT kwa mara ya kwanza litafanyika rasmi  jumamosi hii ya  tarehe 30 mwezi mei katika ukumbi wa Dar Alive –Mbagala,  kuanzia saa kumi na mbili jioni.

Tamasha hili limeandaliwa na Juma nature akishirikiana na EFM kwa lengo la kuwaburudisha Mashabiki wa juma nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka kumi na sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo  Juma Nature aingie kwenye game ya Muziki nchini Tanzania.

Aidha, mashabiki watapata burudani kutoka kwa kiroboto  ambaye atatumia dakika 180 akiwa jukwaani kuhakikisha anakonga nyoyo za mashabiki wake ambapo ataimba nyimbo zake zote kali zilizofanya vizuri na kusindikizwa na wasanii kibao.

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na  Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi.

Tunatoa wito kwa mashabiki wote wa juma nature , Efm Radio, wadau na wengine kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha hili ili kupata burudani hii ya kihistoria ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 7,000 tu.

Tunaamini Juma nature ni msanii mwenye kipaji kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi kipya.

Lakini kwa Efm huyu ni msanii wa Kwanza itaendelea kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwakuwa kwetu sisi tunaamini Muziki unaongea. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

IMETOLEWA NA, DENIS SSEBO,
MENEJA MAWASILIANO NA MAMBO YA SHERIA WA EFM.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment