HUYU NDIE MTOTO ALIYEBEBWA NDANI YA BEGI NA KUSAFIRISHWA KUENDA HISPANIA.

Mtoto aliyebebwa ndani ya sanduku
Mtoto mmoja wa miaka minane amesafirishwa hadi nchini Uhispania kutoka Morroco akiwa ndani ya sanduku kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Uhispania.
Mvulana huyo kwa jina Abou alipatikana ndani ya sanduku hilo lililokuwa limebebwa na msichana wa miaka 19 kuelekea Cueta,eneo lililo karibu na taifa la Morrocco siku ya alhamisi.
Wakati polisi walipolifungua sanduku hilo, mvulana huyo alikuwa katika hali mbaya sana.Mvulana huyo kutoka Ivory Coast sasa anahudumiwa na mamlaka ya Cueta.
Gazeti la Uhispania El Paris liliripoti kwamba msichana huyo wa miaka 19 hana uhusiano na mtoto huyo na kwamba alilipwa na babaake ili kubeba sanduku hilo.
Babaake mtoto huyo anaishi katika visiwa vya Conary na kwamba alitarajia kuonana na mwanawe kulingana na gazeti hilo.
Mtoto aliyebebwa ndani ya sanduku
Chombo cha habari cha Uhispania Efe kimesema kuwa babaake mvulana huyo ambaye anajulikana kama Abou alisafiri hadi nchini Ivory Coast kumchukua mwanawe baada ya kuhamia katika eneo la Gran Canaria mwaka 2013.
Babaake baadaye aliripotiwa kumlipa raia huyo wa Morocco ambaye alimsafirisha mtoto huyo kupitia sanduku.
Msemaji wa polisi aliiambia Efe:''Alionekana kusita na kama ambaye hakutaka kupitia mpakani''.
                            Source BBC Swahil.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment