AKI NA UKWA WA BONGO WAELEZEA MAFANIKIO YAO KWENYE TASNIA YA FILAMU

Kushoto ni Meya Shabani a.k.a Aki akiwa na Mwenzake Nicholaus Ngoda a.k.a Ukwa nje ya ofisi yao
 Aki na Ukwa wa Bongo wakipiga kazi ...
 Hapa wakionesha upande mwengine wa ofisi yao ya International Film Angels

Wasanii wa komedi maarufu kama Aki na Ukwa wa Bongo Muvi wameelezea mafaniko yao kwenye tasnia ya filamu za vichekesho nchini kwa mara ya kwanza tangu wajiingize kwenye filamu mwaka 2010.

Wakizungumza na Komedi Zone, Meya Shabani ambaye ni 'Aki' na Nicholaus Ngoda 'Ukwa' wamesema kuwa moja ya mafanikio waliyoyapata mpaka sasa ni kufanya kazi chini ya kampuni yao ya International Film Angels iliyopo Mwananyamala Visiwani jijini Dar na kuigiza muvi nzuri za vichekesho ambazo zina hadhi ya kipekee kimwonekano na hata simulizi zake tofauti na muvi nyingi za komedi ambazo hukosa ubora unaostahiki.

Baadhi ya muvi zao za komedi walizozifanya ni kama vile; Sometimes Yes Sometimes No, Zero Brain, Lost Sons, Crazy in Hospital, Ayubu wa Leo na Pastor Miyamba's Trial huku wakisema kuwa kuna utitiri wa muvi kali zaidi zipo katika matengenezo.

Mbali na muvi hizo wasanii hao wa Komedi waliongeza kuwa kupitia sanaa wameweza kujiendeleza kimasomo katika kozi za kuongoza filamu, kuedit na kuigiza huku muvi zao zikiwatambulisha vyema kiasi cha kufahamika na watu wengi na kupata dili mbalimbali za kuelimisha jamii kupitia kuigiza na kuimba.

"Kwa sasa tunajiita kama 'Edutainmenter' tukiwa na maana ya kuwa ni waburudishaji na waelimishaji kutokana na uwezo wetu wa kuimba na kuigiza hivyo hayo yote kwetu ni mafanikio japo malengo yetu bado ni kufika mbali zaidi," walisema mastaa hao.

Pia kupata taarifa zaidi za wasanii wa Komedi Tanzania  tembelea mtandao wao wa www.komedizonetz.blogspot.com

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment