Mhe. William Lukuvi.
NA RAYMONDI MINJA IRINGA
MSOMI wa Digri ya uhandisi wa kilomo na mtaalamu wa kilimo cha umwagiliaji kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA)Mhandisi Sebastiani Kayoyo (39) anetangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika
jimbo la Isimani kwa tiketi ya CCM linaloshikiliwa na Waziri wa aridhi ,nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi
Akitangaza nia yake hiyo mkoani Iringa juzi Kayoyo alisema kujitosa katika jimbo hilo ni kuhakikisha maendeleo yakiongezeka kwa kasi na kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo.
Kayoyo alisema kuwa siko kwamba mbunge aliyeko madarakani hajafanya mambo ya msingi ila mbunge huyo ameongoza jimbo hilo kwa miaka mingi hivyo ni fursa ya hazina kubwa ya vijana walioko ndani ya chama cha
mapinduzi kuweza kushika hatamu katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika nchii hiii
"Mbunge anayeshikiria jimbo ninamheshimu sana na ameweza kufanya mambo mengi mazuri, hivyo kwa kidemokrasia nina kuwa na Haki ya msingi kikatiba, nitahakikisha naendeleza mambo ya msingi ambayo bado
hajayatekeleza, hii ni pamoja na kuongeza nguvu kwa wananchi wengi waliokosa fursa mbalimbali" kayoyo
Kakoyo ambaye kwa sasa ni mwajiriwa wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa kama muhandisi wa kilimo (Mtaalamu wa zana za kilimoba kilimo cha umwagiliaji )ni mzaliwa wa kijiji cha Tungamalenda kata ya idodi
tarafa uya idodi iliyopo ndani ya Jimbo hilo la Isimani
Alipoulizwa kuhusiana na hatima ya ajira yake endapo ataukosa ubunge,”Mimi ni mtumishi wa serekalina ninajua raratibu zote za utumishi serekali lakini niko tayari kuacha kazi ili kufanyakazi na ndugu zangu
wa Isimani katika kujiletea maendeleo”
Akitaja vipaumbele vyake endapo chama chake kitampa ridha ya kukimbiza kijiti hicho Kayoyo alisema kuwa ataweka msisitizo katika swala la afya , kilimo ,maji safi na salama pamoja na swala la miundombinu ikiwemo Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa kwa kuwa jimbo hilo halijawahi kuwa na lami tangu nchii hii ilipopata uhuru wake
"Nia yangu ni kuona maendeleo ya jimbo hilo yakiongezeka, napenda kuona wananchi ambao asilimia kubwa ni wakulima wakipata fursa za kusafirisha mazao yao nje ya jimbo hilo huku vijana nao wakipata
kuwezeshwa, uongozi ni kupokezana kijiti hivyo kijiti hicho nitakiongoza vizuri na naomba wananchi siku itakapofika ni kutekeleza wajibu" alisema Kayoyo.
Kwa kujitokeza huko kwa Kayoyo kunafanya idadi ya wagombea kutoka chama cha mapinduzi CCM kufikia wawili akiwemo Mbunge wa jimbo hilo, Wiliam Lukuvi ambaye bado ameonyesha nia ya kuendelea kuliongoza huku kwa upande wa chadema mbunge wa viti maamulu Chiku Abwawo pamoja
makamu mwenyekiti wa bavicha Ole Sosopi.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment