Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maafikiano hayo.
Wanahabari wakisubiri kuchukua taarifa hiyo. Na Dotto Mwaibale MKUU wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda amesema Serikali imetimiza masharti ya madereva kwa kuunda kamati ya kushughulikia kero na matatizo ya madereva ambayo inatarajia kuanza kazi yake Ijumaa. Hatua hiyo imekuja baada ya madereva hao kufanya mgomo kwa muda ukiwa na lengo la kushinikiza kutatuliwa kwa madai yao mbalimbali yakiwemo ya kimikataba baina yao na wamiliki wao. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, Makonda alisema kamati hiyo itakuwa ya kudumu ambayo itakuwa ikishughulikia kero na matatizo ya barabarani nchini. Alisema kamati hiyo ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Uchukuzi, Dk.Shabaan Mwinjaka itakuwa na wajumbe mbalimbali kutoka akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wawakilishi watatu kutoka Chama cha Wamiliki wa Mabasi ya Tanzania (Taboa) na Kakoa, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na washiriki watano kutoka chama cha madereva nchini. Makonda alisema lengo la kuteua wajumbe kutoka Serikalini na taasisi hizo ni kutokana na uwepo wa uhusiano mkubwa kati yao na madereva hao. "Watu hawa wataweza kushirikiana vema na kutatua kero hizi kutokana na wao katika shughuli zao zinahusiana moja kwa moja hivyo kuweza kuendesha kamati hii vizuri. "Tunataka watu kushughulikia jambo kabla halijakuwa tatizo hivyo kamati hii itakuwa ikikutana mara kwa mara katika kushughulikia maswala mbalimbali kuhusiana na madereva na barabara kwa ujumla ili kuondoa kero mbalimbali ," alisema Makonda. Baadhi ya agenda zitakazo fanyiwakazi mara baada ya kamati hiyo kuanza kazi ni pamoja na madai ya madereva hao likiwemo la mikataba ambayo inadaiwa kuwa yanamuda wa miaka kumi, kutokuwa na utaratibu wa kuwalipa madereva hata wakipatwa na matatizo. Alitaja agenda nyingine ni za faini sizizo za mpangilio wanazotozwa madereva hao wakiwa kwenye shughuli zao, suala la kurudi shuleni kila wanapohitaji kurinyu leseni zao na kukaa kwenye mizani kwa muda mrefu pamoja na taratibu nyingine ambazo zinakuwa kero katika shughuli zao. Makonda alisema wakati walipowasili Ofisi ya Waziri Mkuu, walikuta wawakilishi kutoka Wizara ya Uchukuzi, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Taboa, Kakoa, Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Wizara ya Kazi na Ajira, ambapo walikaa na kukubaliana kuunda kamati hiyo. Alisema pamoja na uwamuzi huo wa kuunda kamati hiyo Serikali haitachagua wala kuteua wawakilishi kutoka upande wa madereva ili kuwapa fursa madereva hao kuweza kuwachagua watu ambao wanaaamini zaidi. Kutokana na uwamuzi huo wa kuundwa kwa kamati hiyo ya kudumu Makonda alisema hakutakuwa na mgomo tena kwani kamati hiyo itaweza kidhi mahitaji ya kila upande kwa makubaliano ya wajumbe wake. "Leo, asubuhi kama nilivyo waahidi madereva tulikwenda na wawakilishi waio wakiwemo viongozi wao hadi kwa Waziri Mkuu ili kuangalia kama yale tuliyo yahitaji jana yametekelezwa na hapo tuliweza kupata muafaka na kuunda kamati hiyo. "Hivyo kuanzia sasa hakutakuwa na mgomo na hatutakuwa na mgomo tena kwani madai yaetu tunaimani yatafanyiwa kazi ipasavyo.Na ndio maana tukatoa nafasi kwa madereva kuwa na wajumbe wengi zai ili kuwa na nguvu zaidi kuliko wajumbe wengine katika kutatua kero zao," alisema makonda. Makonda alisema kuwa lengo la kuundwa kwa kamati hiyo si kumaliza tatizo hilo bali ni kuzima moto wa milele kwenye kero za madereva wote nchini. Akizungumzia kuhusu baadhi ya viongozi wakiwemo wanasiasa wanaotumia migogoro kama fursa ya kutafuta umaarufu Makonda alisema si jambo jema na kuwataka viongozi hao hususani vijana kujifikiria kutoa msaada katika jamii na si kutafuta umaarufu. "Niwaombe tu vijana wenzangu najua wazee hawatobadilika na badala yake watuangalie vijana tunavyofanya kazi hivyo tuhakikishe kutokuwa kikwazo kwa mwenzake kwa kugeuza kila anachofanya mwenzake ni jambo baya," alisema Makonda. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/) |
0 comments :
Post a Comment