| Mafuriko makubwa yamevikumba vijiji saba kikiwemo kiwanda cha sukari cha TPC na kuathiri miundombinu pamoja na makazi ya watu kujaa maji. |
| Mbunge wa viti maalumu ,Lucy Owenya (Chadema) (kulia)akiwa ameongozana na diwani wa kata ya Arusha Chini ,Rojas Mmari alipotembelea kujionea athari zilizotokana na mafuriko hayo. |
| Mbunge Lucy Owenya akitembelea maeneo yaliyo athirika na mafuriko hayo. |
| Mbunge Lucy Owenya akitizama sehemu ambayo wananchi walilazimika kuibomoa kwa kushirikiana na uongozi wa kiwanda cha TPC ili kuruhusu maji kupita. |
| Eneo lililobomolewa ili kuruhusu maji ya mafuriko kupita. |
| Baadhi ya nyumba zilijaa maji hali iliyowalazimu wahusika kutoa itu vya ndani nje. |
| Wengine walilazimika kuweka vyakula juu ya mabanda ya kuku. |
| Baada ya maji kujaa wengine walilazimika kuhamishia magodoro yao juu ya paa la Choo. |
| Hata vyakula ambavyo vingi vyao vililowa na maji vilianikwa juu ya paa. |
| Mbunge Lucy Owenya akitizama namna ambavyo baadhi ya wananchi walivyoamua kuokoa vitu ya kwa kuianika juu ya paa. |
| Mifugo pia liathirika na mafuriko hayo. |
| Kutokana na hali hiyo Mbunge Lucy Owenya alilazimika kutoa msaada wa chakula kwa waathirika wa mafuriko hayo |
| Mbunge Lucy Owenya akimfariji mmoja ya waathirika wa mafuriko hayo aliyekuwa akilia kwa uchungu baada ya kupoteza vitu vyake mbali,mbali ikiwemo vyeti vya taaluma ya utabibu. |
| Mbunge Lucy Owenya akikabidhi msaada wa chakula kwa wananchi walioathirika na mafuriko hayo. |
| Mbunge Lucy Owenya akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo. |
| Diwani wa kata ya Arusha Chini Rojas Mmari akizungumza jambo mara baada ya wananchi wake kukabidhiwa msaada huo. |
| Afisa mtendaji Utawala wa kiwanda cha sukari cha TPC ,Jafary Ally akizungumza kuhusu namna mafuriko hayo yalivyo athiri kiwanda hicho. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini |
0 comments :
Post a Comment