Head of India Tanzania Center of Excellence in ICT (DIT), Dr. Amos Nungu akiwakaribisha wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), wakufunzi pamoja na walimu waliofika kwenye mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao.(Picha zote na Geofrey Adroph wa pamoja blog).
Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo akimkaribisha Ofisa anayeshughulikia na masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (wa kwanza kutoka kushoto) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao kwa walimu wa vyuo vya elimu
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari akifungua mafunzo kupitia njia ya mtandao iliyoandaliwa na UNESCO yaliyofanyika jijini Dar.
Bi. Eunice Gachoka kutoka Kenya Institute of Curriculum Development akijitambulisha kwa walimu (hawapo pichani) waliofika kwenye mafunzo ya kupitia mtandao.
Daudi Mbona mkufunzi kutoka chuo cha DIT akiendelea kutoa mafunzo kwa baadhi ya walimu walioudhuria mafunzo ya kupitia njia ya mtandao yaliyofanyika kwenye chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) hapa jijini Dar.
Godfrey Haongo mkufunzi kutoka Open University nchini Tanzania akitoa elimu ya njia ya mtandao.
Baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo.
Na Geofrey Adroph,
Pamoja blog UNESCO imeaandaa mafunzo ya uboreshaji wa elimu kwa walimu hususani katika somo la Tehama kwa vyuo mbalimbali vya hapa nchini vinavyotoa elimu ya ualimu.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania yamefanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) ili kuweza kuwapa fursa hiyo waalimu wa vyuo mbalimbali katika ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya Tehama.
Hii inatokana na baada ya mkutano wa viongozi wa vyuo mbalimbali pamoja na wadau wa elimu wa hapa nchini Tanzania hivyo kuona kama kuna mapungufu katika masuala la uelewa na matumizi ya Tehama hasa katika vyuo hivyo.
Baada ya kuona kuna mapungufu hayo UNESCO waliamua kuanzisha mradi uitwao UNESCO-China Funds in Trust Project (CFIT) wakishirikiana na vyuo vya elimu hapa nchini Tanzania waliamua kuanzisha mradi huo kwa malengo makuu matatu ambayo ni kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya ualimu, kuweka mafunzo ya walimu wanapofundisha katika Tehama ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuwanunulia vifaa vya Tehama ambavyo vitasaidia katika kufundishia na kujifunzia, Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo alivitaja vifaa hivyo kwa kuviorodhesha kuwa ni pamoja na kompyuta, Projecta, na Sola ili kuhakikisha hakuna tatizo la umeme katika ufundishaji wa masomo hayo .
Kupitia mradi huo wa (CFIT), UNESCO imeandaa mafunzo ya siku tano kwa walimu wa vyuo vya ualimu kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu hapa nchini Tanzania ili kuongeza ujuzi na ufanisi katika ukuzaji wa Tehama hasa kupitia kwenye njia ya mtandao na pia kuendana na wakati kutokana na mabadiliko pamoja na ukuaji wa matumizi ya Teknolojia Mafunzo haya yaliyoandaliwa na UNESCO yanafanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa ajili ya kuwapa elimu kwa baadhi ya walimu wa vyuo ili kupata uelewa zaidi juu ya Tehama.
Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Daudi Mboma ambaye ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara kutoka (DIT) na Godfrey Haongo kutoka Open University of Tanzania ambao wanajukumu la kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo tofauti hapa.
Waalimu tisa kutoka chuo cha ualimuTabora, waalimu tisa kutoka chuo cha ualimu Monduli , walimu wanne kutoka chuo cha ualimu Morogoro, mmoja kutoka Shule direct, wawili kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso District, pia kuna baadhi ya watakao pata mafunzo hayo wanatokea Wizara ya elimu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano na UNESCO ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo kwa vyuo vya elimu hapa nchini.
Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya Tehama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa mafunzo ya kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa huduma za kitehama katika taifa la Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wa kutoa mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo katika ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo mkubwa wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika kufanya nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.
0 comments :
Post a Comment