DC MPESYA AWAMWAGIA SIFA WAFANYAKAZI MGODI WA BUZWAGI, NI KATIKA SHEREHE ZA KUWAPATIA TUNZO


Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akitoa maelezo wakati wa kumpatia zawadi za kimila, Shuka ya rubega, mkuki na ngao, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (kulia), wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu kwenye kampuni hiyo, na wengine 10 walizawadiwa kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sera mpya ya Acacia ya tabia sita (six desired behavior), kama kipimo cha utendaji bora wa kazi ambapo ni pamoja na kushirikiana na kufanya kazi kwa uwazi, kutambua ubora wa mfanyakazi na kumuwajibisha anapokengeuka, kupanga kazi na kutenda, kufanya kile ulichopanga kufanya, kufanya kazi kwa wepesi, na kujiendeleza ili kuwa bora katika utendaji wa kazi wa kila siku. Katika hotuba yake, Mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa mgeni rasmi, kwenye sherehe hiyo ambayo ilikuwa maalum kuwatunuku wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, na kufanyika Alhamisi usiku wa kuamkia leo Ijumaa Mei 8, 2015, aliwamwagia sifa wafanyakazi wa mgodi huo hususan uongozi mpya chini yaa Brad, kwa kuja na sera mpya ambayo sio tu inawajali wafanyakazi bali pia wananchi wanaozunguka mgodi huo ikiwemo serikali.

Brad katika vazi la kiasili baada ya kutunzwa na wafanyakazi kwa kuleta mabadiliko katika utendaji kazi wa migodi iliyo chini ya kampuni ya Acacia, ikiwemo Buzwagi

Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia udthabiti wa kampuni hiyo, (GM-Organizational Effectiveness), Janet Reuben-Lekashingo, (kulia), akimkabidhi cheti Isack John Nkulu, kwa utumishi wa muda mrefu kwenye kampuni hiyo. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert Rweyemamu

Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi, Blandina Munghezi, (katikati), akipewa cheti cha utumishi wa muda mrefu katika kampuni ya Acacia, inayomiliki mgodi huo

Brad, akimkabidhi tuzo ya ufanyakazi uliotukuka, Hashim Waziri, katukati ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert Rweyemamu

Meneja wa Biashara, (Commercial Manager), wankampuni ya Acacia, Jason Watson, (kushoto), Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Michell Ash, (kulia), na Meneja wa Mgodi wa North Mara anayeshughulikia uthabiti wa Mgodi, (Effectiveness), Solomon Rwangabona, wakifurahia jambo

Michell, akiteta jambo na Rweyemamu, (kulia)

Sehemu ya wafanyakazi waliohudhuria sherehe hiyo

Michell akimpongeza Meneja anayeshughulikia uthabiti wa Mgodi wa Buzwagi, Sanga, kwa maandalizi mazuri ya sherehe hiyo

Brad, akimkabidhi cheti cha kutambua ufanyazi uliotukuka wa Thompson Paraxceed Francis katika Mgodi wa Buzwagi huku Meneja Mkuu wa Mgodi huoi, Filbert Rweyemamu akishuhudia

Wafanyakazi wakipatiwa utaratibu wakati wa kupokea zwadi na tuzo

Brad, akiwahutubia wafanyakzi wake

Meneja Mkuu, Rweyemamu akitoa hotuba yake

Simon Sanga, akitoa hotuba yake na kuelezea utaratibu na vigezo vilivyotumika kuwapata wafanyakazi bora na wale wa muda mrefu

Mpesya, Kushoto), a,kiagana na Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Mgodi wa Buzwagi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Mstaafu Jamal Rwambow, huku Meneja Mkuu wake, Rweyemamu akishuhudia, mwishoni mwa hafla hiyo

Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Kahama Medical Cultural GHroup, wakifanya vitu vyao huku Tumbili (kushoto) nayw akiruka kufuata midundo ya ngoma
Khalfan Said Photojournalist The Guardian Limited, P.Box 31042 Mobile; +255 646-453/+255-653-813-033 Blog:khalfansaid.blogspot.com Website: www.ippmedia.com Dar es Salaam, Tanzania

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment