PHILIP MANGULA AONGOZA MKUTANO WA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM WILAYA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula (kushoto), akihutubia katika mkutano wa wajumbe wa Halmshauri kuu ya CCM, matawi, wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wao na mabalozi wa chama hicho wilaya ya Ilala, uliohusu utekelezaji wa ilani na mchakato wa uchaguzi mkuu uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Asaa Simba.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Asaa Simba akimkaribisha Mangula kuzungumza na wanaccm wa wilaya ya Ilala.
 Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan 'Zungu' akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo hilo mbele ya Mangula na viongozi wengine kwenye mkutano huo.
  Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan 'Zungu' akimkabidhi Mangula taarifa  ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo hilo.
 Makada wa CCM wakiteta jambo nje ya ukumbi wa Hoteli ya Lamada kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
 Wanaccm wakijumuika kuimba kwenye mkutano huo.
 Wanaccm wa wilaya ya Ilala wakiwa kwenye mkutano huo.

 Makada wa CCM Wilaya ya Ilala wakimshangilia mbunge wao, Mussa Zungu kwa kutekeleza ilani ya CCM.
Viongozi wa juu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula amewataka makada wa chama hicho wenye nia ya kugombea ubunge katika maeneo mbalimbali waache kiherehere cha kuanza kujipitisha katika majimbo wakati wabunge wa maenro hayo bado hawajamaliza muda wao.

Mangula alitoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa wajumbe wa Halmshauri kuu ya CCM, matawi, wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wao na mabalozi wa chama hicho wilaya ya Ilala, uliohusu utekelezaji wa ilani na mchakato wa uchaguzi mkuu uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi.

"Nitoe angalizo kwa wale wenzetu wenye nia ubunge kuacha kiherehere cha kuanza kujipitisha majimboni kuanza kampeni kwa waache kufanya hivyo kwani katika majimbo hayo bado kunawabunge waliochaguliwa hawajamaliuza muda wao " alisema Mangula.

Mangula aliongeza kuwa utaratibu wa chama upo wazi hivyo unapaswa kufuatwa na ukifika tutaona ni nani anapaswa kuendelea na ubunge kutokana na kile alichokifanya kutekeleza ilani ya chama au laa.

Aliwata viongozi wa ccm kuanzia ngazi za matawi kujenga tabia ya kufanya mikutano ya mara kwa mara ambayo itasaidia kujulikana kwa kero za wananchi na kuzifikisha serikali kwa utatuzi.

Mangula aliipongeza wilaya hiyo kwa kupata ushindi wa kuzoa viti vyote 28 katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa akazitaka na wilaya zingine kuiga mfano huo.

Mbunge wa Ilala, Mussa Azan 'Zungu' ambaye alikuwa akishangiliwa kila wakati na makada hao wa ccm  alisema jimbo hilo limjitahidi kwa kiasi kikubwa kutekeleza ilani ya chama hicho kwa kuzipatia shule madawati, maji na katika michezo kugharamia timu 35 kuzipa vifaa katika kipindi cha miaka 10 pamoja na kutoa mikopo kwa wananchi wake kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali.

Zungu alitaja baadhi ya changamoto katika jimbo hilo kuwa ni kusumbuliwa kwa wamachinga, mama lishe na mgambo na ukamatwaji wa pikipiki zaidi ya 500 zinazotumika kama bodaboda ambazo zipo kituo cha polisi cha Chang'ombe. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com)

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment