KLUIVERT, DECO, MENDIETA KUWAKABILI AKINA NSAJIGWA KESHO TAIFA

Patrick Kluivert mchezaji wa zamani wa Barcelona
…………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Mashabiki wa soka kesho watawashuhudia wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert, Gaizka Mendieta , Anderson De Soursa “deco” Francesco Coco na Luis Garcia wakionyeshana kazi na wakali wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hii itakuwa mara ya pili kwa watanzania kushuhudia mastaa hao wa zamani wakikipiga kwenye uwanja huo baada ya wale wa Real Madrid waliokuwa chini ya Luis Figo, Christian Karembeu na  Fabio Cannavaro wakicheza kwenye uwanja huo kwa mara ya kwanza na kushuhudiwa na Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikosi cha FC Barcelona kimesheheni wachezaji nyota wengi mbali ya Kluivert na wenzake ambao kwa mashabiki wa soka ni majina maarufu. Wachezaji wengine ambao wanatarajia kushuka leo uwanjani  chini ya kocha maarufu, Johan Cruyff mi pamoja na makipa nyota, Jesus Mariano Angoy Gil na Robert Oscar Bonano.
Wengini ni  Sergi Barjuan Esclusa, Albert Toams Sobrepera, Luis Milla Aspas, Lluis  Carrreras Ferrer, Miguel Angel Nadal Homar, Ion Andoni Goikoetxea Lasa, Oscar Arpon Ochoa, Santiago Ezquerro Marin, Javier Villena Mulero, Magin Civantos Martinez, Mateo Segura Capellades na  Simao Sabrosa.
Kocha wa timu hiyo, Cruyff alisema kuwa wamekuja kuonyesha vipaji vyao vya zamani vilivyotukuka na hakuna wa kuwazuia kushinda katika mechi ya leo. Alisema kuwa wachezaji wake wegi japo wameacha soka, bado wanajihusisha kwa kufundisha na wengine kufanya mazoezi kwa ajili ya timu yao “FC Barcelona Legends”.
“Tupo vizuri, tumejiandaa kwa ajili ya kuweka historia, tunajua wenyeji wataleta upinzani, lakini sisi ndiyo tutakuwa washindi,” alisema Cruyff kwa kifupi.
Mratibu wa mechi hiyo kutoka kampuni ya Primetime Promotion, Stuart Kambona alisema kuwa maandalizi yamekamilika na kikosi cha Tanzania Stars kitakuwa na nyota kama Manyika, Kaseja Shadrack Nsajigwa, Abubakari Kombo, Mustapha Hozza, Salvatory Edward, Amour Aziz, na Yusuph Macho.
Wengine kwa mujibu wa Kambona ni Shaban Ramadhan, Dua Saidi, Nassoro Bwanga, Mohamed Hussein, Steven Nyenge, Mwanamtwa Kihwelu, Edibily Lunyamila, Henry Morris, Haruna Moshi, Bitta John, Madaraka Selemani, Deo Lucas, Bakari Malima, Thomas Kipese, Khatibu Sinapo na Nico Nyagawa.
Kambona alitaja viingilio katika mchezo huo kuwa ni Sh 7,000 kwa viti vya kijani, Sh10,000 (blue), Sh20,000 (Orange), Sh30,000 (VIP C), Sh50,000 (VIP B) na SH300,000 for VIP A

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment