WABUNGE NADHANA YA UWAJIBIKAJI


                                                                   Na Canal Mathias
Ndugu zangu,

Yapo majaribu mengi ambayo katika dunia ya leo yanaranda kila kona, Lakini Shetani anafanya kazi ya ziada kwa kuyaunda walau hata zaidi, Lazima tuwe tunaweza kuwajibikia wakati tunakabiliwa na majaribu ambayo yanatishia maisha yetu ya kiroho.

Biblia inatueleza kwa ufasaha tena weledi mkubwa kuwa hatuna jukumu la kupigana vita visivyo vya kimwili bali vya kiroho dhidi ya nguvu na vikosi vya kiroho ambavyo hututishia (Waefeso 6:12).

Kupitia gazeti la Mwananchi la tarehe 15 Mei 2015 imetolewa Orodha ya wabunge 10 vilaza na wabunge 10 makini, orodha hii imeeleza wazi juu ya Bunge la Kumi ambalo limebakiza mkutano mmoja tu wa bajeti ili wabunge wote kufungasha virago ishara ya kufunikwa kando chororo za uwakilishi wa miaka 5 nikiwa namaana ya kutia nanga jahazi hili lililokuwa na Vilaza nawengine Timamu.

Inajulikana wazi kwenye msafara wa wajanja na wajinga huwa wamo ni kama ilivyo jalala lolote lile halikosi taka kavu na taka laini, Gazeti hili limeeleza wazi kwa lugha ya ufasaha inayotumiwa na Watanzania ambayo ni lugha ya kiswahili kuwa wapo baadhi ya wabunge ambao hawajauliza swali la msingi, swali la nyongeza wala kuchangia chochote tangu kuapishwa kwa mwaka mmoja uliopita ama miaka 5 yote.

Kwanza nimesikitishwa kusikia kuwa Bunge ambalo lina wabunge 358 wawakilishi wa wananchi Tanzania wapo wabunge ambao hawajawahi kabisa kuchangia ikiwa ni pamoja na wale wawili waliotajwa gazetini ambao ni pamoja na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi Mohamed Said Mohamed (CCM) ambaye ni mwakilishi wa Mpendae na Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili,pamoja na mbunge wa Kitope (CCM), Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Hivi unawezaje kuwa mbunge ambaye hafikishi matatizo ya wananchi wake au wanasubiri vikao vya ukoo ili waeleze matatizo ya familia zao? Ni swali tu najiuliza hata wewe unaweza nisaidia kupata majibu ili tuwe sawa katika tafakuri.

Yupo mbunge mwingine wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri (CCM) ambaye amechangia mara nne...Duh hatuwezi kuendelea na utaratibu kama huu wa kuwa na vilaza bungeni kazi yao iwe ni kusinzia na kukunja posho tu za watanzania ambao bado wameshindwa kuwawakilisha vyema kama walivyotegemea.

Ebooo!... Hata kijana mwenzangu niliyetegemea atawakilisha kwa uzuri wananchi wa Jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa nae eti yupo kwenye 10 vilaza loooh inasikitisha sana wananchi kuchagua watu waliowekewa plasta mdomoni.

Lakini yawezekana hoja zingine sio kila mbunge anaweza kuchangia bungeni mana uchangiaji wa mambo unahitaji weledi mkubwa kujua mambo ya kisheria, uchumi, kijamii, kiutamaduni, na siasa safi ikiwa ni pamoja na mambo ya yahusuyo taifa zaidi sana lazima mbunge uwe mfatiliaji wa mambo otherwise ataongea yote Kombo kama mtoto ajifunzaye kuzungumza.

Lakini zipo hoja zingine zinawazidi upeo wao maana wengine walipita kwa kuokoteza kura na wengine walipita kwa potelea mbali, hii mbaya sana kama tunachagua wabunge ambao hawawezi kabisa kuuliza swali hata la nyongeza basi walau wawashe hata maiki tu waseme Ndiooooo au Hapanaaaaa ili tujue wapo.....Looolooooo kumbe wananchi waliwatuma kusema Ndio au Hapana!.

Yupo mjumbe mmoja katika kujadili haya alinambia kuwa tatizo kubwa linalowafanya wabunge wengi kushindwa kuchangia ni kwakuwa wapo chama Tawala hivyo wanakosa uhuru wa kuikosoa serikali,
la Hasha kwa mtazamo wangu mimi hii haiwezi kuwa sababu hata tone kwani kila kitu ukichangia bungeni unaikandia serikali mbona yapo mambo yawahusuyo wananchi mazuri tu ambayo hata serikali haiwezi kukulaumu kuwa ameibemenda.

No! No! Nakataaa kata kata uvivu na ukilaza wa wabunge wetu ndio tatizo la kushindwa changia hoja, Hapa uwajibikaji upo wapi kwa wabunge wetu au wamekwenda kushangaa ukumbi wa bunge mjini Dodoma na mitaa yake?

Naam, Hii ni Taswira ya wabunge na Dhana ya uwajibikaji kwa kuwa wabunge wachache tu wanaowajibika lakini wengi wao hakuna jipya.

Ni Neno La Wakati Mwema
Mathias Canal
0756413465

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment