KAMANDA LIBERATUS SABASI:ENDELEENI NA SHUGHULI ZENU HAKUNA HOFU YA UGAIDI ARUSHA

…………………………………………………………………………
Mahmoud Ahmad Arusha.

HALI  ya hofu miongoni mwa wananchi wa Mkoa wa Arusha imejitokeza,
jana asubuhi, kufuatia kusambaa kwa ujumbe mfupi kwenye mitandao ya
kijamii na simu za kiganjani kuwa kuna magaidi wanne  wamekamatwa na
silaha aina ya SMG katika chuo cha Uhasibu Njiro (IAA).
Akizungumzia taarifa hizo,Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Liberatus
Sabasi, alisema wananchi wanapaswa kuendelea na shughuli zao kama
kawaida na kupuuza ujumbe huo.
“Ujumbe huo ulikuwa na lengo la kuwatia hofu wananchi ila sio kweli na
sisi watu w aulinzi na usalama tumeimarisha ulinzi ,watu wafanye kazi
zao kama kawaida,”alisema.
Alisema taarifa hizo zitakuwa zimesambazwa na wahuni wachache kwa
lengo wanalojuwa wenyewe.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda, akizungmza na waandishi wa habari ofisini kwake
alisema huo ni uwongo na kila mmoja aupuuze kwani unaweka wananchi kwenye wakati mgumu wa kufanya majukumu yao.
“Mimi nipo katika kikao sasa hivi cha kamati ya ulinzi na usalama,
hizo taarifa za uwongo na uzushi mkubwa watu wazipuuze,”alisema.
Alisema kuwa taarifa hizo ni uzushi mtupu hiyo wananchi wawe na amani kufanyashughuli zao za kujiletea maendeleo bila hofu yeyote na kuwa jeshi la polisi limejipanga kila kona ya mkoa kuhakikisha unakabiliana na matukio yeyote ya kiuhalifu
Aliwataka wamiliki wa mahoteli yote pamoja na wenyeviti wa mitaa na vijiji kuhakikisha wanakuwa makini kwa wageni wote wanoingia kwenye sehemu zao ilikuwatambua watu wote na kuhakikisha wanaorodhesha majina ya wageni hao kama taratibu za kuhakiki ikiwa ni pamoja na kuangalia vitambulisho vyao.
“Natoa wito kwa wamiliki wa mahoteli kuhakiki majina ya wageni na kutomuachia mgeni kujaza fomu pekee na pia kuhakiki kitambulisho chake na anatokea wapi pia wenyeviti wa vitongoji,vijiji na mitaa kuhakikisha wageni wote wanaoingia kwenye maeneo yao wanawatambua”alisema mkuu wa mkoa.
Alisema kuwa mipaka yote ipo salama hivyo wameweka ulinzi kwenye maeneo hayo ya mipaka ya nchi yetu kwa mkoa wa Arusha kwenye maeneo ya namanga na Loliondo
Naye Afisa habari wa Chuo cha Uhasibu Njiro, (IAA), Sarah Goroi,
akizungumza kwa njia ya simu ya kiganjani, alikanusha uvumi huo na
kudai wanafunzi wanaendelea na masomo kama kawaida.
“Taarifa hizo hazina ukweli wowote, tunaomba wafunzi waendelee na
masomo yao kwani huo ni uzushi,”alisisitiza.
Kwa upande wa Afisa Uhusiano Mwandamaizi  wa Chuo cha Ufundi
Arusha,(ATC) , Gasto Leseiyo, alisema kwa chuo chao katika kukabiliana
na magaidi tayari wamefunga kamera maalum za kutambua wahalifu na sasa
wameanz akuzifunga maeneo ya nje ya chuo baada ya kukamilisha kazi
hiyo ndani ya chuo.
Mmoja wa wakazi wa Jiji la Arusha, Samweli Mollel, alisema kuwa
taarifa hizo zisipuuzwe zifanyiwe kazi, kwani hali ya usalama sasa ni
tete na wananchi lazima wawe na mashakam kutokana na kilichotokea
Garisa nchini Kenya.
Mapema asubuhi jana, kulitembea ujumbe wa maneno  kwenye simu za
mkononi, ukidai kuwa maafisa usalama Arusha, usiku wa kuamkia jana,
wamekamata watu wanne wakiw ana gari aina ya Premio nyeusi ikiwa na
bunduki SMG 4 na risasi 160, wakijaribu kuingia chauo cha Uhasibu
Njiro kw amadai ya kutaka kusalimia mwanafunzi mmoja wa kike ambaye ni
ndugu yao na wakatiliwa mashaka na kutiwa mbaroni.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment