OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA MAKUMBUSHO YA TAIFA WATOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI MKOA WA DAR ES SALAAM KUHUSU MUUNGANO WA TANZANIA NA ZANZIBAR

Ofisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa, Anamary Bagenyi (kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo hayo. Kushoto ni Ofisa Ustawi wa Jamii, Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Elimida Kashuna.
Ofisa Ustawi wa Jamii, Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Elimida Kashuna (katikati), akizungumzia mafunzo hayo mbele ya wanahabari.
Wanafunzi wakiigiza igizo linalohusu muungano.
Wanafunzi wakiwa kwenye warsha hiyo.
Wadau mbalimbali na walimu wakiwa kwenye warsha hiyo.
wanafunzi hao wakifurahia warsha hiyo.


ZAIDI ya Watoto 1,200 kutoka shule 42 za mkoa wa Dar es Salaam wamepatiwa mafunzo kuhusu Muungano wa Tanzania na Zanzibar ambapo maadhimisho ya miaka 51 yanatarajiwa kuadhimishwa Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa na Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa Anna Mary Bagenda wakati akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo.

Bagenda alisema wanafunzi hao wa shule ya msingi wamepatiwa mafunzo mbalimbali kuhusu muungano ambapo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo na ufahamu kuhusu tendo hilo.

Alisema wamelazimika kuchukua wanafunzi wa shule za msingi kutokana na ukweli kuwa vijana wengi kwa sasa wanaoneka kukosa ufahamu wa muungano.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Elimida Kashumba alisema utaratibu huo wa kuwapatia wanafunzi elimu utakuwa endelevu kwa kila mwaka.

"Matarajio yetu ni kuhakikisha kuwa utaratibu huu unakuwa endelevu kwa nchi nzima ili wanafunzi waweze kujua muungano wao ni vipi," alisema.

Alisema iwapo vijana na watoto wa shule ya msingi watapata elimu ni wazi kuwa uelewa wa muungano utakuwepo wakutosha," alisema.

(Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habari za jamii.com/)










About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment