Mwenyekiti wa Chama cha Mapindizi CCM mkoa wa Iringa Jeska Msambatavangu amefananishwa na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu Edwadi Lowasa kwa kuwa na moyo wa kusaidia makundi mbalimbali katika jamii
inayomzunguka bila ya kuangalia itikadi za vyama wala udini.
Kufuatia kujitoa kwake jumuiya ya Wanafunzi Waliookoka (PSI) mkoani Iringa Imesema itampa tuzo ya heshima Mwenyekiti huyo wa Chama kama ile tuzo aliyopewa Lowasa na askofu wa kanisa la Overcomers la mjininhapa ikiwa ni kama ishara ya kumtia moyo kwa michango yake mbalimbali ya kimaendeleo anayotoa katika jamii.
Tuzo hiyo ya hesima iliyokuwa itolewe katika kusanyiko kubwa la wanafunzi hao lililofanyika katika shule ya sekondari ya wasichana Iringa, imeahirishwa hadi waati mwingine kutoka na sababu zilizoelezwa ni kutokuwepo kwa viongozi wa kubwaz wakiroho ambao walikuwa hawajafika mwaka huu.
Mmoja wa viongozi wa jumuiya hiyo, Revocatus Senje alisema; “tumeahirisha kukupatia tuzo hii na zawadi nyingine hii leo kwasababu kusanyiko la leo halijahudhuriwa na makundi yote yaliyotarajiwa.
“Nina diriki kusema kuwa huyu mama ni kiongozi shupavu anayetumia fedha zake nyingi kusaidia makundi mbalimbli bila ya kuwabagua kwa itikadi licha ya kuwa yeye ni kiongozi wa ccm mimi binafsi na mfananisha na mheshimiwa lowasa kwani naye amekuwa mstari wa mbele kusaidia watu mimi namuombe siku moja aje kuwa kiongizi mkubwa kama ninavyomuombea lowasa aje apate hata apate ubunge ili aje kukomboa
vijana wa iringa ”
Senje alisema jumuiya hiyo imepanga kufanya kusanyiko lingine kubwa katika Chuo Kikuu cha Iringa (IUCo) wakati wowote kuanzia sasa; kusanyiko linalotarajiwa kuhudhuriwa na wachungaji, viongozi, wazazi, walimu, walezi na wanafunzi wanaounda jumuiya hiyo.
“Tunakupa zawadi hii kama ishara ya kuukubali upendo wako kwa jumuiya yetu na makundi mengine na kwa kuzingatia kwamba umekuwa ukiisaidia mara kwa mara unapoombwa kufanya hivyo,” alisema.
Akizungumzia moja ya michango ya Msambatavangu kwa jumuiya hiyo, Senje alisema mapema mwezi huu alichangia jumla ya Sh Milioni 2 ili kuwezesha jumuiya hiyo kuendesha kambi yake ya Pasaka, iliyofanyika
kati ya April 1 hadi 5 katika shule ya sekondari Kitwiru, mjini Iringa.
Akishukuru kwa ahadi hiyo, Msambatavangu alisema; “ni wajibu wetu kama wazazi kuwalea vijana wetu ili wakue katika njia inayompendeza Mungu.”
Alisema vijana wanatakiwa kuwa kielelezo cha Taifa lenye maadili mema na wakatae kutoa nafasi kwa watu wanaowadharau kwasababu ya fedha zao, vyeo au umaarufu.
“Mnatakiwa kukua huku mkujiua kwamba bidii yenu itawafanya myapate hayo yote ambayo wengine wanayatumia kuwadharau,” alisema.
Katika kusanyiko hilo wana jumuiya hiyo walipata fursa ya kujadili mada iliyohusu ‘uongozi unaobadilisha ni uongozi ambao mtu anayepewa dhamana na Mungu anaweza kuleta mabadiliko yaliyokusudiwa.
0 comments :
Post a Comment