MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AVALIA NJUGA TATIZO LA UBOVU BARABARA WILAYANI KWAKE

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.
……………………………………………………….
UCHUNGUZI JUU YA UBOVU WA BARABARA ZA WILAYA YA KINONDONI 13.04.2015
UTANGULIZI
Ndugu waandishi wa habari na ndugu wananchi, nimewaiteni leo, kuwaambia juu ya Agenda moja tu. Nayo ni Ubovu wa barabara.
Tangu
sijaingia ofisini hapa, na baada ya kuingia ofisi hizi za umma, kila
siku Napata fursa ya kuzunguka maeneo mbalimbali katika maeneo ya
Kinondoni, nimekuwa nikisiliza jamii nzima ya Kinondoni, wengi kero yao
kubwa ni ubovu wa barabara nchini lakini hasa wakiinyooshea kidole
wilaya yangu ya Kinondoni. Mimi nitazungumzia ubovu huo katika wilaya
yetu hii ya Kinondoni. 

Wananchi wamekuwa wakilalamika juu
ubovu wa barabara, wanasema barabara zinajengwa chini ya viwango, kiasi
lami inawekwa leo lakini haimalizi miezi sita inabanduka na inaacha
mashimo. Kwamba mashimo yamekuwa ni sehemu ya maisha ya kawaida ya
barabara zetu hapa Kinondoni. Mitaro haipitishi maji kama
inavyotakikana, Mitaro mingine inachimbwa mifupi kuliko mahitaji halisi,
barabara zinakuwa nyembamba kutoka kushoto kwenda kulia, pia wembamba
kutoka chini ya lami hadi juu (Surface area). Kwamba ujenzi wa barabara
katika Wilaya yetu hauendani na kasi ya mahitaji na kukua kwa mji.
Wananchi wana ichallenge Seriklai kuwa inawezekana kasi ndogo ya
kujengwa wka barabara za WIlaya inatokana na sababu kuwa kila siku
tunakarabati barabara badala ya kujenga kwa ubora ili tupanuwe wigo wa
huduma! Wapo wananchi wanaohoji iweje ubovu huu wa barabara uachwe hivi
hivi kiasi serikali ipo na haioni kama kuna tatizo. 
Jambo hili
limenistuwa, nikaona mengi ya madai haya na mengine ambayo sijayaeleza
yana msingi, na nikasema si busara kuwaacha wananchi wananung’unikia
hali hii ili hali wao wenyewe ndio walipa kodi wakuu. Hawa wananchi wana
haki ya kujuwa thamani halisi ya fedha ambayo ni kodi yao je inalingana
na gharama halisi ya miradi ya ujenzi?
DHIMA HALISI
Sasa
mimi binafsi si mtaalamu wa masuala ya Uandisi wala usanifu, nikasema
hili suala ni lazima tulichukulie kwa umakini na tulipatie majawabu,
hivyo basi nimeunda tume huru ya wataalamu, itakayojumuisha Wasanifu,
Waandisi, wataalamu wa Mikataba, wataalamu wa Ugavi na Manunuzi na watu
wengine kutoka vyombo vyetu mbalimbali vya uchunguzi ili wakachunguze
pamoja na mambo mengine, usanifu wa barabara zetu kama unazingatia
viwango, taratibu za manunuzi na kutoa tenda kama zinazingatiwa,

wakandarasi wetu wazalendo kama wanawajibika ipasavyo au kuna njama
yeyote inafanywa ili kuhujumu kazi wanazopewa, je waansishi wetu
wanatimiza wajibu wao ipasavyo katika mchakato mzima wa usanifu na
ujenzi ili kuhaklikisah ubora wa barabara unafikiwa?
MATOKEO YA TUME
Tume
hii itafanya kazi kwa siku 21 kuanzia tarehe 15.04.2015 na kukabidhi
ripoti yake tarehe 5.May.2015 saa 4:00 asubuhi ofisini hapa, mbele yenu
waandishi wa habari. Matokeo ya ripoti hiyo ndiyo itakayotoa majibu wa
ama tupanuwe wigo wa uchunguzi mpaka kwenye kandarasi zingine za ujenzi
wa shule za serikali, ofisi za umma za Wilaya au la, Majibu yatapatikana
baada ya kupata taarifa hii.

Ninaamini kwa
njia hii ya uwazi na ukweli majibu ya haki juu ya kilio cha wananchi
yatapatikana. Ili kubaini chanzo na ukubwa wa tatizo. Majibu hayo
naamini hayatamuumiza mtu isipokuwa tu kama anahusika na ubadhirifu na
uzembe utakaobainika.

WAJUMBE WA TUME
1)Eng. Julius Mamilo Contractor Specialist – National Construction Council NCC – Mwenyekiti
2) Eng. Ronald Rwakatare Road Fund Department of Value for Money- Katibu
3) John Malisa – Cental Milo Laboratory – (CML)Mjumbe
4) Abednego Lyaga – Procurement Specialist – Mjumbe
5) Eng. Patrick Balozi (Engineers Registration Board) – Mjumbe
Na wajumbe wengine wawili kutoka vyombo vingine vya serikali vinavyoshughulika na uchunguzi.
Terms of Reference zimeambatinishwa kwa rejea yenu ambayo kamati itaifanyia kazi.
Imetolewa na
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment