Etoile kutua Tanzania usiku wa manani

Etoil du Sahel
Wapinzani wa Yanga timu ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia wanatarajiwa kuwasili saa 9 usiku kuamkia Ijumaa kwa usafiri wa Ndege ya kukodi ya kampuni ya Nouvelair bj 4870 wakiwa na msafara wa watu 56.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tunisia (FTF), Krifa Jalel ndiye mkuu wa msafara huo akiwa na Rais wa klabu ya Etoile du Sahel (ESS) Charefeddine Ridha, wachezaji 19, benchi la ufundi lenye watu 13, waandishi wa habari 12 na wanachama 10
Timu ya Etoile du Sahel itafikia katika hoteli ya Ledger Plaza zamani Bahari Beach eneo la Kunduchi, na Ijumaa wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Waamuzi wa mchezo huo ni Samwel Chirindiza, Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe, Jose Maria Bachide wote kutoka nchini Msumbuji na walitarajiwa kuwasili mchana wa Alhamisi, huku kamisaa wa mchezo huo Salah Ahmed Mohamed kutokea nchini Sudan akitarajiwa kuwasili leo jioni na wote watafikia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment