KATIBU wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,amekanusha taarifa zilizopo kuwa chama hicho kinakisaidia Chama cha ACT Wazalendo akidai kuwa hawana sababu ya kufanya hivyo.
Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Nape zinasisitiza kuwa CCM hakina sababu ya kusaidia chama kingine cha siasa hivyo uvumi huo ni uchafuzi wa kisiasa.
Akizungumzia kauli ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema, Dk Wilbroad Slaa,kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza kuandikisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ngome ya CCM alisema huo ni upotoshaji uliokubuhu kwani tanzania nzima ni ngome ya chama hicho.
Alisema ratiba ya NEC haijapangwa kimkakati kama alivyodai Dk Slaa na kila mtanzania ataandikishwa kwa mujibu wa sheria hivyo kauli za kuwapotosha na kuwapa hofu wananchi hazina mashiko. "Kauli hizi za Dk Slaa mzee kama yule ni uthibitisho tosha kwamba wenzetu vyama vya upinzani hasa chadema siasa zao zina lengo la kuwagawa watu kikanda,kanda wanayoiona ni kaskazini, uthibitisho wa mbegu mbaya ya chuki," alisema Nape
Alisema CC.M wanalaani vikali siasa za namna hiyo kwani hizo sio hoja za msingi ila ni za kuwagawa wananchi na kupandikiza chuki zisizokuwa na maana na suala hilo linaonyesha jinsi wapinzani wanavyofanya siasa za kikanda.
"Tunayo taarifa kwamba Dk Slaa,Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe pamoja na Mwenyekiti wa Nccr-Mageuzi,James Mbatia walikaa vikao wakawatenga wenzao wanaunda Umoja wa Katiba Mpya (Ukawa, ambao ni Mwenyekiti wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba ambaye anatokea Tabora na DK Emmanuel Makaidi ambaye anatoka Kusini, hao wote tunajua wanatoka mikoa gani,"alisema Nape
Nape alisema siasa za namna hii zinazigawa nchi na kinachoonekana ni kwamba wapinzani wanajua kuwa watashindwa na ccm ndio maana wanatafta sababu,hivyo anawatoa hofu wananchi kuwa kila mtu mwenye sifaa ataandikishwa.
"Chadema wanajua watawaangusha vibaya, hatuna mpango wa kutumia mizengwe watanzania watatuchagua, waache kuwagawa watanzania kwa kutaka madaraka, wanatakiwa kuwashawishi wananchi kujiandikisha kama CCM tunavyofanya"alisema Nape
"Wanapandikiza mbegu mbaya na chuki yenye lengo la kugawa watanzania,nchi hii ni moja ina makabila 136 na tunaishi vizuri hizi siasa chafu hazifai,, maneno ya hovyo ambayo hayastahili kusemwa na mtu mzima kama yule, watashindwa ndio maana wanasema watu wanaandikishwa kiujanja ujanja, wameanza kujenga mbinu za ajabu, wananchi wanatupenda na watazidi kutuchagua,"alisema Nape Alivitaka vyama vya siasa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na waliache zoezi hilo liende kama lilivyopangwalilivyopangwa, wasiwajengee watu hofu, hii sio sawa.
0 comments :
Post a Comment