SEREKALI YABARIKI UJENZI WA KITUO CHA MAFUTA KWENYE CHANZO CHA MAJI

                                                                                 NA RAYMOND MINJA IRINGA

UJENZI wa Kituo cha Mafuta cha Kampuni ya Puma Energy Tanzania Ltd uliokuwa ukipingwa na wadau mbalimbali kwa madai kwamba unajengwa katika eneo oevu la Mto Ruaha Mdogo, mjini Iringa, umeruhusiwa
kuendelea.

Mapema Februari mwaka huu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa ililazimika kuiandikia kampuni hiyo barua ya kusimamisha ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa katika kiwanja namba 30/1 Kitalu A Ndiuka, mjini Iringa,
baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa walioitwa wadau.

Akizungumza na wanahabari jana, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amesema baada ya kupokea malalamiko hayo, Desemba 12, mwaka jana ofisi yake ilimwandikia barua Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Binilith Mahenge  ili aje kusaidia kutoa ufafanuzi kwa
walalamikaji.

Masenza amesema kuwa Waziri alimtuma Mkurugenzi wa Baraza la Mazingira la Taifa, NEMC aliyetoa maelezo ya kina juu ya mchakato wa kutoa cheti na kuruhusu ujenzi wa kituo hicho.

Walalamikaji hao ambao hata hivyo hawakutajwa, walikuwa na hofu ya usalama wa maji na mazingira ya mto huo endapo kituo hicho kitajengwa.

Maji ya mto huo kwa mujibu wa Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazigira (Iruwasa),  Marco Mfugale ndiyo yanayotegemewa na wakazi wa manispaa ya Iringa na vitongoji vyake kwa matumizi mbalimbali
yakiwemo ya majumbani.

Sababu nyingine inayodaiwa kutolewa na walalamikaji hao ni hofu waliyonayo kwamba kituo hicho kinaweza kuwa chanzo cha ajali za magari kwa kuwa kinajengwa jirani na barabara kuu ya Tanzam na ile
inayopandisha mjini Iringa.

Masenza amesema ili kuhakikisha ujenzi na uendeshaji wa kituo hauathiri mazingira, Machi 13, mwaka huu uongozi wa mkoa uliitisha kikao cha wadau katika mradi huo ili NEMC pamoja na mwekezaji watoe
ufafanuzi wa hoja walizonazo wadau kuhusiana na ujenzi huo.

Wadau waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na uongozi wa mkoa na kamati yake ya ulinzi na usalama, uongozi wa manispaa pamoja na wataalamu wake, Meneja na Wataalamu wa Tanroads, wataalamu kutoka Bonde la Mto
Rufiji, Iruwasa, NEMC na mwekezaji.

Katika kikao hicho, Masenza alisema wadau walipata nafasi ya kuhoji mambo mbalimbali waliyokuwa na wasiwasi nayo hususani uchafuzi wa maji ya mto huo.

Kwa kupitia utafiti wa ki-haidrojia uliofanywa na NEMC kupitia Dk Ibrahim Mjema wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ulithibitisha kuwa hakutakuwa na uchafuzi wa maji ya ardhini.

Alisema kituo kitajengwa nje ya eneo la hifadhi ya barabara kuu ya TANZAM na ile inayoingia mjini Iringa huku magari yanayoingia na kutokea kituoni yatafanya hivyo kupitia barabara ya TANZAM.

Amesema kuwa  kuzingatia uchunguzi liofanywa na ripoti ya tathimini ya athari kwa mazingira, uongozi wa mkoa umeridhika na mradi huo kutokana na tahadhari zote zilizochukuliwa na zitakazoendelea kuchukuliwa na
mwekezaji hivyo wamemruhusu kuendelea na ujenzi wake.     

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment