Ikiwa ni siku mbili tu zilizopita serikali wilayani Babati mkoani Manyara ikianza kutafakari namna ya kusaidia kaya 50 zilizoezuliwa na kipupwe kilichoambatana na mvua kubwa katika kata ya Nkaiti, tayari wilaya hiyo imeendelea kukumbwa na jinamizi la mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku na kusababisha kubomoka kwa nyumba 10 huku kaya zaidi ya 80 zikilazimika kuyakimbia makazi yao kufuatia kuzingirwa na maji katika mji mdogo wa magugu.
ITV ilifika katika maeneo ya mitaa ya mnadani na majengo "B" ya mji huo wa magugu na kushughudia gharika ya maji yaliyozingira kaya hizo ikiwa ni pamoja na kanisa la mungu na shule inayofundisha michepuo ya kiingereza huku baadhi ya familia zikinusurika kifo na kulazimika kuhamia kwenye baadhi ya madarasa ya shule ya chekechea, lakini wakisema huenda mafuriko hayo yamesababishwa na udogo wa calvat ama kuziba kwa kalvati lililojengwa kwenye barabara kuu kwani limeshindwa kupitisha maji mengi kwa wakati mmoja.
ITV ilipata kuzungumza na baadhi ya familia zilizokosa makazi baada ya nyumba zao kubomolewa na mafuriko hayo, huku wakiiomba serikali kukimbiza msaada wa haraka wa chakula na misaada ya dharura kwani wamepoteza kila kitu, huku wengine wakiitaka serikali kuifanyia marekebisho sehemu ya barabara hiyo.
Nae afisa tarafa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maafa ya tarafa hiyo ya mbunge Bw Gitu Sedoyeka amesema bado hali ni tete endapo wananchi hawatachukua hatua za haraka za kuondoka katika maeneo hayo, huku kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw Hassani Lugendo akiwataka wananchi kusaidiana kabla ya kuanza kwa jitihada za serikali.(KILONGE)
0 comments :
Post a Comment