Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akiwahutubia wanaccm wa Kata ya Sinza katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kufuatia kukipa ushindi chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Cholaje akihutubia katika mkutano huo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia), akielezea mafanikio ya maendeleo ya wilaya hiyo pamoja na changamoto zilizopo. Kushoto ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Cholaje.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Sinza, Salum Kabuda, akihutubia kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (katikati), akimkabidhi kadi Mariam Ally aliyejiunga na jumuiya hiyo. Jumla ya wananchi 28 walijiunga na jumuiya hiyo na kukabidhiwa kadi zao pamoja na kul kiapo. Wananchi waliojiunga na jumuiya ya wazazi Kata ya Sinza wakila kiapo mbele ya mgeni rasmi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge.
Baadhi ya viongozi wa CCM nao wakishiriki kuapa wakati wanachama wananchi waliojiunga na jumuiya hiyo wakiapa.
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
wananchi na wanaccm wakiwa kwenye mkutano huo.
Taswira ya mkutano huo. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com |
0 comments :
Post a Comment