Bingwa wa magonjwa ya mwili wa binadamu, Dk. Meshack Shimwela akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Kelvin Twissa akijibu maswali ya wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Dk. Sulende na Dk. Shimwela (kushoto).
Wanahabari na wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano na Madaktari Bingwa.
KAMPUNI ya mawasilianao ya Vodacom Tanzania imezindua huduma mpya itakayowawezesha watumiaji wa mtandao wa kampuni hiyo kupata taarifa muhimu kuhusu afya kwa siku 30 mfululizo bila malipo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Simu Dokta, Dk. Meshack Shimwela ambaye ni Bingwa wa magonjwa ya binadamu (Physician), alisema upatikanaji
wa taarifa sahihi za kiafya ni moja kati ya hatua muhimu za kupambana na magonjwa mbalimbali.
Dk. Shimwela alisema huduma hiyo itatoa mchango mkubwa katika kuuhabarisha umma juu ya masuala muhimu ya kiafya na kuongeza kuwa ujumbe wa mara kwa mara utawakumbusha watu na namna
ya kujikinga pamoja na kuchukua hatua sahihi juu ya magonjwa.
Aidha Dk. Shimwela aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuzindua huduma hiyo kwa ajili ya umma na kusema kuwa ‘’ Inaendana na malengo ya milenia hasa namba sita linalosisitiza kupambana na
magonjwa mbalimbali, akiwataka Watanzania kuitumia huduma hiyo ambayo ni muhimu kwa kila mtu’’.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania , Kelvin Twissa alisema taarifa hizo zitakuwa katika mfumo wa ujumbe mfupi wa maneno (sms) na mteja atakuwa
akizipata kila siku kupitia simu yake ya mkononi bure kwa mwezi baada ya kujisajili kwa kutuma neno DAKTARI kwenda 15542.
‘’Lengo la huduma hii ni kuchochea na kusaidia wananchi kujua mambo mbalimbali ya kiafya ambayo wamekuwa hawayajui au kuwa na taarifa zisizo sahihi, taarifa hizo zitakuwa zikiandaliwa na madaktari
bingwa nchini wa magonjwa mbalimbali ambao wamejitolea kuelimisha jamii, pamoja na kusaidia ustawi wa jamii kwa kuwa na jamii yenye uelewa mkubwa wa mambo ya afya na kusaidia kuokoa maisha ya
watu wengi,’’ alisema Twissa.
Hii itakuwa ni huduma ya kwanza ya aina yake kutolewa na Vodacom ikiwahusisha madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kwa kutoa taarifa kila siku za kuwasaidia kujiepusha na maradhi au kutoa
ahueni kwa magonjwa yanayowasumbua.
Madaktari hao bingwa ni pamoja na Dk. Meshack Shimwela (Bingwa wa magonjwa ya mwili wa binadamu (Physician). Dk. Sulende Kobhoja (Bingwa wa watoto na moyo (Paediatricia & Cardiologist), Dk.
Munawara Kaguta (Bingwa magonjwa ya wanawake/wajawazito (OBST/Gynecologist).
(Picha na Gabriel Ng’osha/GPL)
-----
JINSI YA KUJIUNGA
0 comments :
Post a Comment