Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migoro(kulia ) akimkabidhi cheti Kaimu Balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsu naga ikiwa ni ishara ya kutambua msaada wa nchi hiyo wa kuisaidia Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika hatarishi ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati wa sherehe ya mahafali ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika jana.
………………………………………………………………………………
Na Magret Kinabo, MAELEZO
UBALOZI wa Japan kupitia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje umetoa kiasi cha fedha cha Sh. Milioni 800, ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani 500,000 kwa ajili ya kusaidia Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA Nakayama, iliyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Balozi wa Japan chini, Kazuyoshi Matsu naga wakati wa sherehe za mahafali ya pili ya shule hiyo yaliyofanyika jana na kuhudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro ambaye alikuwa mgeni rasmi baadhi ya viongozi , wakiwemo baadhi ya wake za viongozi na wagemi wengine mbalimbali.
“ Juzi Idara ya Mambo ya nje ya Japan imekubali kutoa Dola za Marekani 500,000 kwa ajili ya mradi wa mpya wa awamu ya pili wa kusaidia shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama,” alisema Kaimu Balozi huyo.
Matsu naga aliongeza kwamba fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kompyuta na utawala, yakiwemo mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Matsu naga aliongeza kwamba fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kompyuta na utawala, yakiwemo mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
“Sisi Wajapan tunapenda kuendelea kutoa msaada kadri inavyowezekana. Msaada wa leo utaongeza urafiki kati nchi ya Japan na Tanzania,” alisisitiza.
Kaimu Balozi huyo alimataka kila wanafunzi wa shule hiyo, kutoa mchango wake katika kuleta maendeleo ya jamii kwa kutumia mafunzo aliyoyapata.
Kwa upande wake, Dkt. Migiro, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, aliwataka wadau mbalimbali kuendelea kumsaidia Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete katika kusaidia wanafunzi hao ili kupanua fursa za watoto wa kike kielimu.

“Nimegundua kuwa mtoto wa kike anakabiliwa na upungufu wa fursa si kitaaluma. Hivyo kuchangia shule hii kwa mtoto wa ni kujenga na kuihimarisha ya fursa yake yeye binafsi na familia kwa ujumla.
Dkt. Migiro alifurahishwa uweleadi wa wanafunzi wa shule hiyo, yakiwemo mazingira bora, ambapo alisema shule hiyo inaviwango bora.
Dkt. Migiro alifurahishwa uweleadi wa wanafunzi wa shule hiyo, yakiwemo mazingira bora, ambapo alisema shule hiyo inaviwango bora.
Naye Mke wa Rais Mama Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka wanafunzi hao kutumia nafasi ya kusoma bidii ili waweze kufaulu hatimaye kushika nafasi mbalimbali za uongozi kama Dkt.
Akizungumzia kuhusu matarajio ya WAMA kutokana shule hiyo, alisema kutoa wataalamu wa nyanja zote , ikiwemo fani ya sayansi . Hivyo aliwataka kuongeza bidii katika masomo ya sayansi.
Alisema WAMA itaendelea kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hadi watakapofikia hatua ya mwisho.
Alisema WAMA itaendelea kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hadi watakapofikia hatua ya mwisho.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi (TAMISEMI) Hawa Ghasia aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa bidii zao ambao zimeifanya shule hiyo kuongeza katika wilaya hiyo.
Jumla ya wanafunzi wapatoa 89 wanatarajiwa kuhitimu elimu ya kidato cha nne mwaka huu katika shule hiyo.
Jumla ya wanafunzi wapatoa 89 wanatarajiwa kuhitimu elimu ya kidato cha nne mwaka huu katika shule hiyo.
0 comments :
Post a Comment