TPB YAKABIDHI MADARASA NA OFISI SHULE YA MSINGI MSENJELELE.

Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Gregory Teu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (kulia) wakizinduwa madarasa na ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi Msenjelele.
Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Gregory Teu (kushoto) akimkabidhi cheti maalum cha shukrani Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (kulia) mara baada ya kukabidhi madarasa na ofisi ya walimu iliyojengwa kwa msaada na benki yake (TPB).
Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, Gregory Teu pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (wa kwanza kulia) wakishirikiana kuzinduwa vyumba vya madarasa pamoja na ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Msenjelele. Majengo hayo yamejengwa kwa msaada na Benki ya Posta Tanzania.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msenjelele walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa madarasa yao wakiwa katika picha ya pamoja. Nyuma yao ni sehemu ya jengo la madarasa na ofisi za walimu zilizojengwa na TPB kwa msaada.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (kulia) akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi Msenjelele katika hafla ya uzinduzi wa vyumba vya madarasa pamoja na ofisi Shule ya Msingi Msenjelele.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (wa tatu kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Gregory Teu (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni na wanafunzi walioshiriki hafla hiyo ya kukabidhiwa ofisi na madarasa.
                                                                    Na Mwandidhi Wetu, Dodoma.


BENKI ya Posta Tanzania (TPB) kupitia tawi lake la Dodoma, imejenga madarasa mawili pamoja na ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi Msenjelele ikiwa ni jitihada zake za kukuza elimu nchini na kupambana na madhari ya ujinga na umaskini kwa Wananchi wa Kijiji cha Chunyu Mpwapwa.


Akikabidhi msaada huo katika Kijiji cha Chunyu Mkoani Dodoma jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi alisema benki yake ilichukua jukumu la kusaidia ujenzi wa madarasa hayo na ofisi ya walimu baada ya kuguswa na kitendo cha wanafunzi kutembea umbali mrefu hasa wale wenye umri mdogo kutembea umbali mrefu kwenda kijiji jirani kuifuata huduma ya elimu.


Alisema TPB iliguswa na umbali wa zaidi ya kilomita 12 ambazo wanafunzi walilazimika kutembea kila siku kwenda shuleni kijiji cha jirani na Kijiji cha Chunyu. Alisema mara baada ya kupokea ombi lakusaidia ujenzi huo toka kwa uongozi wa Kijiji cha Chunyu walikubali na kuanza ujenzi huo.


Alisema ujenzi huo wa madarasa pamoja na ofisi ya walimu yaliojengwa kisasa umeigharimu Benki ya Posta Tanzania kiasi cha shilingi milioni 50, hivyo kuwaomba wanafunzi na wananchi wa eneo hilo kuyatunza na kuyatumia vyema ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.


Kwa upande wake Mbunge wa Mpwapwa Gregory Teu, akipokea msaada huo wa majengo aliishukuru Benki ya Posta Tanzania kwa moyo wao wa ukarimu na upendo waliouonesha kwa wananchi wa Kijiji cha Chunyu ambao walikuwa wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa.


Alisema kwa upande wake alikuwa akiguswa na kero hiyo ya wananchi wake waliyokuwa wanaipata hivyo kuamua kutafuta ufadhili wa kujengewa madarasa kutoka kwa taasisi mbalimbali. “..Naishukuru Benki ya Posta kwa kuitikia wito huo mara moja na bila kusita,” alisema Mbunge huyo.


Alitoa wito kwa wanakijiji cha Chunyu kuhakikisha watoto wao wanakwenda shule sasa na kufuatilia maendeleo yao ili kukuza ufaulu na kujenga kizazi chenye msingi mzuri wa elimu watakao kuja kuwa viongozi bora wa kesho.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment