Bw.Hassan Mtenga
CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa chakishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) kwa kuwazuia wanachama wake mjini Iringa kunywa maziwa ya Asas Dairies Ltd
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga alisema kuwa hatua ya Chadema kuwazuia wanachama wake mjini Iringa kunywa maziwa ni dalili mbaya kwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa mwaka 2015.
Kwani alisema kuwa kuwazuia wanachama wao kunywa maziwa ni moja ya hatua ya kuwataka kufa kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwani maziwa ni tiba tosha kwa watu wenye matatizo na wasio na matatizo.
Mtenga alisema kuwa maziwa ya Asas Dairies Ltd hayana uhusiano wowote na chama chochote cha siasa na kuwa hatua ya viongozi wa chadema kuacha kuzungumzia kazi ambazo mbunge wao Msigwa amefanya na kuelekeza mapambano yake katika maziwa si siasa bali ni kuishiwa hoja za kuwaeleza wananchi.
“Tunashangazwa sana na uwezo wa uelewa wa viongozi wa Chadema hivi kweli inaingia akilini kiongozi ama chama kumzuia mwanachama wake kunywa maziwa ama kula ? kweli ni kufirisika kisera maana bila mtu kula atakufa na nani atakupigia kura ” alihoji Mtenga .
Hata hivyo alisema kuwa hakuna asiyetambua kuwa wapo wafanyabiashara ambao ni wanachama wa Chadema kama hivyo ndivyo basi CCM kuwatangazia wanachama wake kuwa wasinunue wala kuingia katika maduka ama kupenda bidhaa za wafanyabiashara ambao ni wanachama wa Chadema nchini.
Alisema kuwa kuwa kawaida chama kina mpaka yako katika kuwaongoza wananachi na wananachi ama wanachama wana uhuru wa kupenda chochote bila kuvunga sheria .
Hivyo alisema kuwa chadema wanapaswa kuwaomba radhi wananchi wa jimbo la Iringa kwa kauli hiyo ambayo ni sawa na kumzuia mtu kula ama kuishi vinginevyo CCM kinawataka wananchi kupuuza kauli hiyo ambayo imelenga kuwaondolea haki ya kuishi .
Pia alisema iwapo wanachama wana biashara zao si vema vyama kuhusisha biashara ya mtu na itikadi za vyama na kudai kuwa viongozi wa chama wapo kwa ajili ya kuvuruga biashara za watu .
CCM kimetoa kauli baada ya viongozi wa chadema Iringa mjini na makamu mwenyekiti wa baraza la vijana Taifa (BAVICHA ) Patrick Sosopi kutumia mkutano wake wa hadhara kuwazuia wananchi kunywa maziwa hayo ya asas kwa kudai kuwa mmoja kati ya wanafamilia wa mmiliki wa kampuni hiyo anasaidia CCM Iringa .
0 comments :
Post a Comment