JE, WAJUA KITI KINAWEZA KUKUTOA UPWEKE? HIKI NDIO KITI KINACHO PUNGUZA UPWEKE.

      Kuna wakati kila mmoja maishani pengine huhitaji kupata 'hug' (kukumbatiwa) ili kujisikia sio mpweke. Sasa kampuni moja nchini Japan imetengeneza kiti maalum ambacho kitakuwa tayari wakati wowote kumkumbatia na kumliwaza mtumiaji.

Kiti hicho cha "utulivu" kimetengenezwa kikiwa pamoja na 'mdoli' mkubwa mwenye sura yenye tabasamu pamoja na kofia, lakini muhimu zaidi ana mikono mirefu ambayo inaweza kumkumbatia mtumiaji.
"Inakufanya ujisikie salama. Kila mtu anaweza kutumia, lakini zaidi kimeundwa kwa ajili ya wazee," amesema msemaji wa UniCare, kampuni inayouza kiti hicho.


Karibu robo ya idadi ya wananchi wa Japan kwa sasa wana umri wa zaidi ya miaka 65, idadi ambayo inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 40 katika miongo kadhaa ijayo.
Kiti hicho kinauzwa kwa yen 46,000 sawa na dola 419.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment