Meneja wa mradi wa CIRDA kutoka UNDP, Bonizella Biagini akizungumza wakati akitambulisha maofisa waliokuwepo katika uzinduzi wa warsha ya siku tatu ya kimataifa ya ukusanyaji na matumizi ya taarifa ya hali ya hewa kwa nchi 12 duniani. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Mipango ya maendeleo duniani (UNDP) Phillippe Poinsot, Mwakilishi wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge, Bw. Richard Muyungi.
Na Mwandishi wetu.
MATAIFA 11 ikiwemo Tanzania yanakutana jijini Dar kwa mafunzo ya siku tatu yanayohusu utengenezaji wa mifumo bora ya upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa,uchakataji wake na matumizi ya taarifa hizo kwa wananchi wa kawaida na watunga sera ili kuwa na uhakika na Mipango ya maendeleo.
Mataifa hayo ni yale yalioyopo katika mradi wa Multi Country Support Programme to Strengthen Climate Information Systems in Africa (CIRDA).
Nchi zinazohusika katika mpango huu pamoja na wenyeji Tanzania ni Benin, Burkina Faso, Ethiopia, the Gambia Liberia, Malawi, Sierra Leone, Sao Tome and Principe,Uganda na Zambia.
Mpango wa CIRDA unafadhiliwa na Global Environment Facility (GEF) na Least Developed Country Fund (LDCF) ukilenga kuwezesha utumiaji wa teknolojia mpya miongoni mwa wakulima, watunga sera na sekta binafsi ili kuweza kufanya maamuzi sahihi kwa kuzingatia taarifa sahihi za hali ya hewa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkazi wa UNDP,Phillippe Poinsot Mpango wa CIRDA, ambao ni mfano wa kuigwa kwa juhudi za mataifa ya Afrika ya kuwa na ubadilishanaji wa maarifa na taarifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, huzingatia uhusishaji wa sekta binafsi, matumizi ya simu na takwimu za kilimo (agricultural index insurance).
Akifungua mafunzo hayo, kwa niaba ya waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa rais, mazingira Binilith Mahenge, Ofisa anayeshughulikia mradi huo nchini Richard Muyungi alisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo dunia nzima iko katika changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabianchi.
Alisema Mafunzo hayo ambayo yanazinduliwa nchini yatajenga uwezo wa wataalamu wa kubadilishana maarifa ili kuona kwamba wananchi wanafaidika na utaalamu uliopo.
Alisema Tanzania ikiwa inategemea zaidi wakulima katika uchumi wake ufikishaji wa taarifa za hali ya hewa katika ngazi za chini na kwa usahihi ni muhimu.
Alisema program ya CIRDA ni mwenedelezo wa juhudi za serikali ya Tanzania katika kushirikiana na mataifa mengine, kuimarisha mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kw akuongeza uwezo na weledi miongoni mwa wananchi wake na wadau wa hali ya hewa.
Kutokana na hali hiyo Muyungi, alisema Tanzania inafuraha kufanyakazi na UNDP kwa lengo la kuhakikisha kwamba taarifa za hali ya hewa na hadhari ya awali ya uwapo wa majanga zinawafikia wananchi na zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Ndugu Abbas Kitogo Afisa Miradi ya Mabadiliko Tabia nchi kutoka UNDP akijitambulisha kwa washiriki wa warsha.
Kwa mujibu wa Muyungi Tanzania inashirikiana na UNDP kuboresha upatikanaji wa takwimu zinazotakiwa za hali ya hewa ili kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewani katika sekta za maendeleo.
Warsha hiyo inayofanyika katika hoteli ya Whitesands imelenga kutoa na kubadilishana utaalamu wa namna ya kuhudumia wananchi kupitia data zinazotolewa na mamlaka za hali ya hewa na taasisi za kukabiliana na majanga.
Akisisitiza umuhimu wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Philippe Poinsot ambaye alimwakilisha mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodrigues alisema uzinduzi wa programu hiyo umelenga kuimarisha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa na hadhari za awali za majanga kwa manufaa ya wananchi wa mataifa hayo.
Mwakilishi wa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge, Bw. Richard Muyungi akifungua mafunzo hayo ya siku tatu kwa wataalamu wa hali ya hewa, mabadiliko ya tabia nchi na wanaojihuisha na majanga kutoka nchi 12 ikiwemo Tanzania katika mpango wa CIRDA.
CIRDA ni mpango wa kiutafiti wa mfumo wa hali ya hewa na mabadiliko yake unaozingatia upatikanaji wa data za hali ya hewa na kuzifikisha maeneo husika kwa matumizi kwa wakati.
Mradi huo umelenga kuhakikisha wakulima, watunga sera na sekta binafsi wanafanya maamuzi kwa kuzingatia taarifa za hali ya hewa kutokana na mabadiliko makubwa yaliyopo sasa.
Mabadlikiko ya tabia nchi yamefanya nchi nyingi kukumbwa na hali ya hewa mbaya kwa maana ya kuvuruga uasili wa mazingira na kusababisha adha katika kilimo na uvuvi.
Mafunzo hayo yamelenga kuangalia teknolojia iliyopo sasa na namna ya kutumia teknolojia hiyo kutoa tija katika kutengeneza na kutathmini taarifa za hali ya hewa kwa lengo la kuimarisha mipango ya maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi mkazi wa UNDP Philippe Poinsot akihutubia katika warsha hiyo.
Mapema mwakilishi wa UNDP Tanzania alisema Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo zinaathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa na mafunzo yatasaidia kuepuka adha za mabadiliko ya hali ya hewa kwa wananchi vijijini hasa kwa kuzingatia kwamba wananchi wake wengi wanategemea kilimo.
Alisema kukosekana kwa taarifa za hali ya hewa kunafanya wananchi waliopo vijijini kutokuwa na uhakika na maendeleo yao na kuwa katika hatari ya kuyumbishwa na majanga mbalimbali.
Alishukuru kwamba wataalamu wa kimataifa wanafanyakazi na serikali ya Tanzania kwa lengo la kuhakikisha kwamba taarifa za hali ya hewa zinapatikana na kutumiwa kusaidia mipango endelevu. (1) Ndugu Abas Kitogo Afisa Miradi ya Mabadiliko Tabia Nchi kutoka UNDP Akijitambulisha kwa washiriki wa warsha.
Washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza mada kwa makini.
Ndugu Pascal F.Waniha mwakilishi wa mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa akitoa mada wakati warsha hiyo.
Meza kuu wakipiga makofi.
Mmoja wa watoa mada Jeremy Usher kutoka CIRDA akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa takwimu na uangaliaji wa mifumo katika dunia inayokabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ndugu Richard Muyungi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
0 comments :
Post a Comment