MHE. HALIMA MDEE NA WENZAKE WALIVYOPELEKWA GEREZA LA SEGEREA BAADA YA KUNYIMWA DHAMANA.

Mbunge wa Kawe Halima Mdee (kulia), akionesha alama ya mbili inayotumiwa na Chadema wakati akisindikizwa na polisi kwenda kupanda gari kuelekea gereza la Segerea Dar es Salaam jana baada ya kunyimwa dhamana na wenzake kutokana na kesi inayomkabili ya kufanya maandamano yaliyozuiliwa na jeshi la polisi.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, akipanda gari la Polisi Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam jana, wakati akipelekwa Gereza la Segerea.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimalisha ulinzi katika Mahakama ya Kisutu.
Hapa Halima akisindikizwa kupanda gari.

 Baadhi ya wanachama wa Chadema, waliokuwa na Halima wakiwa ndani ya gari la polisi kabla ya kupelekwa segerea wakionesha alama ya mbili inayotumiwa na chama hicho.
Gari lililombeba Halima na wenzake 

likiondoka Mahakama ya Kisutu.
Wanachama wa Chadema wakishangilia nje ya 
Mahakama ya Kisutu.

Dotto Mwaibale

MBUNGE wa  Jimbo la Kawe Halima Mdee (35) amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za  

kutotii amri halali ya Jeshi la Jolisi na kufanya mkusanyiko usio halali.  

Wakili wa Serikali Mkuu Bernard kongola akisaidiana na Salum Mohamed na Hellen Mushi 

alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi  Janeth Kaluyenda wa Mahakama ya Hakimu Mkazi 

Kisutu, Dar es Salaam kuwa Mdee anakabiliwa na mashtaka mawil

Kongola alidai mbali na Mdee washtakiwa wengine ni Rose Moshi (45), Renina Peter 
Anna Linjewile(48), Mwanne KAssim (32), Sophia Fangel (28), Edward Julius (25), Martha 

Mtiko (27) na Beatu Mmari (35) wote wa kazi wa Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa Oktoba 4 mwaka huu washtakiwa wakiwa mtaa wa Ufipa, bila kuwa na 

uhalali walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP) Emmanuel 

Tillf kwa niaba ya Jeshi la Polisi.

Kongola alidai washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 124 cha Sheria ya 

Kanuni ya Adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Alidai katika shtaka la pili washtakiwa hao wakiwa eneo hilo hilo, walifanya mkusanyiko usio 

halali kwa lengo moja la kutembea kwenda kwenye Ofisi ya Rais huku wakijua ni kinyume 

cha sheria.

Wakili  huyo alidai kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 74 na 75 cha Sheria ya Kanuni 

ya Adhabu, sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka yao walikana kuhusika na tuhuma hizo. 

Upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo waliiomba 

mahakama kupanga tarehe ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH).

Hakimu Kaluyenda alisema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana wanatakiwa kila mmoja 

asaini bondi ya sh. milioni 1  kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja kati yao awe 

anafanyakazi katika taasisi inayotambulika kisheria.Mdhamini huyo awasilishe barua kutoka 

kwa muajiri wake na kitambulisho cha kazi.

Upande wa Mashitaka umeiomba mahakama kuwapa nafasi ya kwenda kukagua nyaraka za 

dhamana zilizowasilishwa na wadhamini wa washtakiwa hao.

Hakimu ameiahirisha kesi hadi Oktoba 21, 2014 itakapokuja kwaajili ya washtakiwa hao 

kusomewa maelezo ya awali.

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment