Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakiongoza msafara katika safu ya milima ya Usambara kwenda Jimbo la Mkinga, Tanga.
Nyuma ya Nape ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Majid Mmanga na nyuma ya Kinana ni Mhariri wa Habari wa gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe.
Mbele ni Kinana na Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa gazeti la Uhuru, Seleman Jongo.
Kinana mbele na kutoka kushoto ni wanahabari walio kwenye msafara huo, David John wa Majira, Seleman Jongo wa Uhuru na Said Mwishehe wa Jambo leo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Majid Mmanga.
Nape akiwasili katika Kata ya Mg'aro mpakani mwa Wilaya ya Lushoto na Mkinga. Pia Kata hiyo inapakana na Kenya.
Kinana na Nape wakifuahi baada ya kuwasili salama baada ya kutumia usafiri wa baiskeli.
Nape akihutubia wananchi katika Kata ya Mg'aro mpakani mwa wilaya za Lushoto na Mkinga.
Kinana akihutubia katika Kijiji cha Mg'aro ambapo aliwahakikishia wananchi wa eneo hilo kuwa barabara ya kutoka Lushoto kwenda Mkinga itaboreshwa, halafu na umeme utawekwa katika Kata hiyo.
Kinana akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto baada ya msafara wake kukabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mkinga katika Kata ya Daluni.
Kinana akiangalia ngoma ya utamaduni iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Daluni, wilayani Mkinga.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Zahanati katika Kijiji cha Daluni, wilayani Mkinga.
Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika Kata ya Maramba.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Kituo cha Polisi Maramba.
Wananchi wakishangilia huku mmoja wapo akiwa na bango la kuisifia CCM katika mkutano huo wa hadhara.
Kinana akizawadiwa mswala uliotolewa na wanakijiji.
PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
0 comments :
Post a Comment